Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:06 pm

NEWS: ABDALLAH MTULIA ANYAKUA UBUNGE KILAINI, APITA BILA KUPINGWA

Dar es Salaam: aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF na baadae kutimkia CCM Abdallah Mtolea, amepita bila kupingwa baada ya msimamizi wa tume ya uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi hii ni baada ya wagombea wengine waliochukua fomu ili kuwania kiti hicho kukosa sifa.

Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mtolea amekiri kupita bila kupingwa.

Katika hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge ambayo Mwananchi imeiona inaeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 81 (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Mtolea amechaguliwa kuwa mbunge wa Temeke katika uchaguzi uliofanyika leo.

Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).