- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEW: MSIGWA AKANUSHA TAARIFA ZA KUHAMIA CCM
Iringa: Mbunge wa Iringa mjini(CHADEMA) Peter Msigwa amekanusha vikali uwepo wa taarifa za yeye kutaka kuhamia chama cha Mapinduzi CCM na kusema kuwa taarifa hizo ni zauzushi na wazipuuze.
Akiongea Jana Agosti 3 kupitia ukurasa wake wa twitter msigwa alisema "Nimesikitishwa sana na propaganda alizozifanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo(jana) wakati anawaapisha wakuu wapya wa wilaya katika mkoa wake za kuuaminisha umma kuwa najiandaa kuhamia CCM hizo taarifa ni uzushi na wana IRINGA MJINI na Wafuasi waamifu wa CHADEMA wazipuuze mimi bano nipo sana CHADEMA"
Kwa zaidi ya wiki moja mfululizo wanasiasa ikiwemo wabunge na madiwani kutoka vyama vya upinzani CUF na Chadema wametangaza kujiengua katika vyama vyao ikiwemo kujiuzulu nafasi zao za uongozi na kutimkia CCM.
Naibu meya wa manispaa ya ilala, na diwani wa vingunguti Omari kumbilamoto amejiuzulu nafasi ya udiwani na umeya lakini pia amejivua uanachama wa CUF.
Mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga Laizer amejiuzulu na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Kabla ya kalanga kujiuzulu alikuwa ni mwanasiasa wa upinzani, Mwita Waitara alitangaza kujiengua katika chama kikuu cha upinzani cha chadema na kujiunga na Chama tawala, CCM.
Waitara aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga lililopo Dar es salaam alikishutumu chama cha Chadema, kuwa hakina demokrasia pia kutokuwa na maelewano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Ikumbukwe kuwa wabunge hawa wote yaani Waitara na Kalanga waliwahi kuitumikia CCM, ambapo Waitara aliitumikia CCM mwaka 1998 mpaka mwaka 2008 wakati Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM.
Hata hivyo baada ya kujiengua baadhi yao wamepata neema ya kuteuliwa na rais katika baadhi ya nafasi za uongozi. Wiki iliyopita Rais Magufuli alimteua David Kafulila kuwa katibu tawala wa mkoa wa Songwe.
Awali Kafulila alikuwa mbunge wa chama cha upinzani NCCR-Mageuzi.
Pia alimteua Moses Machali kuwa mkuu wa wilaya ya Nanyumbu. Kabla ya uteuzi huo Machali aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu mjini kupitia NCCR-Mageuuzi ambapo baadaye alihamia ACT-Wazalendo kisha kwenda CCM.
Mwanasiasa mwingine aliyepata fursa hiyo ya kuteuliwa na Rais ni Patrobas Katambi ambaye amekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma, Kabla ya hapo Katambi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chadema.