- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MKURUGENZI NEWALE "TUMEJIPANGA HAKUNA KOROSHO ITAKAYO INGIA KUTOKA NCHI JIRANI"
MTWARA: kurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema kuwa Halmashauri ya Newala ni moja ya Halmashauri zinazopakana na nchi jirani ya Msumbiji ambapo kwa upande wa majirani zetu kwa sehemu nao wanalima zao la Korosho hivyo wamejipanga kwa kila namna kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kuwa hakuna korosho kutoka nchi jirani itakayopenya nchini kupitia milango ya Wilaya hiyo.
Mkurugenzi Newala
amesema kuwa tayari askari wa JWTZ Wamejipanga katika Maghala na wameimarisha ulinzi kwa kukagua na kulinda korosho hili isije mtu akatokea akatia doa wilaya yake kwa kufanya vitu tofauti na maagizo ya Rais.
Aidha Chimae amesema tangu kutangazwa kwa operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala wamezunguka Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho yote nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari asubuhi leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae amesema kuwa wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote.
"Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa kutoka nchi jirani," alisema Chimae.