Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:36 pm

MANENO YA NUH MZIWANDA YAZUA UTATA KWENYE NDOA YA SHILOLE

Dar es salaam: Jana usiku Majira ya Jioni Ndoa ya mwanadada Mwajuma Mohamed A.K.A Shilolele amefunga ndoa na mpenzi wake wa hivi karibuni Asharafu Uchebe alimaarufu kama Uchebe, Saa chache baada ya ndoa hiyo aliyekuwa mpenzi wa zamani wa shilole Nuh Mziwanda amezua utata kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti moja ya line ya wimbo wa Hamisi Mwinjuma alimaarufu kama Mwana FA kwenye ngoma yake ya Bado nipo nipo kwanza iliyoachiwa miaka takribani 7 iliyopita, Nuh ameandika kuwa wasichana wote wanadangaya maisha yao kwahiyo yeye bado yupo yupo "Alie LaLa na BiBi harusi'wiki Moja KabLa ya harusi'Na wala sio Bwana Harusi'Bado mnanishauri harusi (all girls are pretenders )" aliandika Nuh

Nuh Mziwanda amekuwa mpenzi wa Shilole kwa miaka kadhaa, waliachana na mrembo huyo baada ya Nuhu kumuoa msichana mwingine anayeitwa Nawali Masoud ambapo ndio msichana walie zaa nae.

Ndoa ya Shilole na Uchebe imefanyika jana usiku Majira ya saa 1 nyumbani kwake Meneja wa Diamond platnumz Babu Tale mikocheni jijini Dar es salaam na baada ya ndoa hiyo akamchukua mume wake na kumpeleka nyumani kwake kwa shilole.

Ndoa ya shilole haikuudhuriwa na Dada yake shilole anaye ishi hapa jijini Dar es salaam ambaye hakuwa tayari kushiriki katika harusu hiyo ambapo kwamujibu wa shilole mwenye anasema kuwa ndoa hiyo haiwezi kutofungwa kwa sababu ya Dada yangu kwani yeye sio mama yangu kwa hiyo hawezi nipangia mimi mambo yangu" aliongea shilole wakati akihojiwa na Sudi Brown

kwa mujibu wa shilole mwenyewe amesema wamepanga Tarehe 20 Dec 2017 ndio siku itakayo fanyika sherehe ya Harusi hiyo.