Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 6:51 am

MAKALA : USAJILI ULIOFANYA VYEMA MPAKA SASA LIGI KUU BARA

i

Msimu wa ligi kuu bara 2017-2018 umeingia katika mwaka mwingine wa pili wa 2018,zipo timu ambazo zilisajili nyota wakutosha kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao katika sehemu tofauti,wapo wachezaji ambao wameanza vyema pindi waliposajiliwa na wapo ambao mpaka sasa bado hakijaeleweka

mategemeo ya makocha mbalimbali yamekuwa tofauti kwa baadhi ya wachezaji baada ya kuwasajili na hawana masaada wa kutosha mpaka sasa,ila baadhi ya nyota wanaonekana kufanya vyema na wakati ligi inaenda nusu ya muhula yaani mzunguko wa 15 tayari baadhi usajili mpya umeonekana kuwa na tija na kufanya vyema katika timu zao na ligi kwa ujumla

Ditram Nchimbi ( Njombe Mji fc)

Pamoja na simba kuifunga Njombe Mji fc goli nne kwa bila katika mchezo uliofanyika uwanja wa uhuru,lakini mabeki wa simba watakwambia Ditram ni mtu wa aina gani,ingawaje hasikiki sana kwenye midomo ya watu,ila anafanya vizuri na timu yake ya Njombe Mji fc,alionekana kivutio kwa mbeya city akiwa na majimaji,na baada ya kuitumikia Mbeya city kwa miaka miwili akahamia Njombe Mji fc ambako huenda baada ya muda tukamuona sehemu nyingine ya juu zaidi.

Danny Usengimana ( Singida United )

Ni mshambulaiji ambaye aliibuka kinara cha kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Rwanda,na kwasasa ni mchezaji wa singida United,aliifungia bao pekee timu yake katika mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Lipuli fc ,Usengimana anasajiliwa akitokeo Polisi fc ya Rwanda,hivyo ameonekana kuteka wapenzi wengi wa soka kutokana na ubora wake awapo uwanjani

Emmanuel Okwi ( Simba )

Anaweza kucheza kama winga au kiungo mshambuliaji,hakuna asiyemjua mchezaji huyu kwa umahili wake wa kutikisa vyavu na kuhadaa mabeki wa kila timu pinzani,aliwahi kucheza simba kwa miaka kadhaa na kutimikia yanga kabla ya kwenda kucheza soka nje ya nchi,katika urejeo wake ligi kuu bara uongozi wa klabu ya simba uliamua kumrejesha nyumbani na tayari mpaka sasa yeye ndiye mfungaji bora wa ligi kuu bara

Papy Kabamba Tshishimbi ( Yanga )

Alisajiliwa na Yanga akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland,ni mkongo ambaye amejizolea umaarufu ndani ya muda mchache,umaarufu wake umekuja kutokana na namna anavyoweza kukaba kwa wakati,kupandisha mashambulizi na kupiga mipira ya uhakika nafikiri ukimuuliza Omog Tshishimbi ni nani,basi mnunulie soda kwanza kisha akupe stori yake ipasavyo

Mbaraka Yussuph ( Azam fc )

Yanga iliweka mezani dau kubwa zaidi kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyu wa zamani wa Kagera Sugar,lakini akaikacha na kutimkia Azam ni mchezaji mwenye umri mdogo ambaye anaweza kutikisa nyavu vyema,pia alitwaa taji la mchezaji bora chipukizi kwa mwaka 2017,ni mzuri katika kupunguza mabeki wa timu pinzani,amekuwa na msimu mzuri akiwa na azam akiongoza safu ya ushambuliaji iliyoachwa na john Bocco.

Aishi Manula ( Simba )

Wanapenda kumuita "Tanzania One"nafikiri hili jina halijaja kwa bahati mbaya limekuja kulingana na uwezo wake wa kuhakikisha mpira hauvuki mstari wa goli kirahisi,ni mlinda mlango tegemeo kwenye kikosi cha Taifa stars na klabu yake ya Simba,alianza kujizolea umaarufu tangu aliposajiliwa akiitumikia Azam fc ni aina ya kipa ambaye kumfunga kwake lazima ufanye kazi ya ziada.

Wazawa wako sawa na wageni

Uwiano wa wachezaji wazawa na wakigeni katika kufanya vizuri unaonekana kuwa haupo sawa kwa maana wazawa wengi wanaonekana kuanza kuangunga kulinganisha na wageni ambapo mpaka sasa walioonekana kuteka midomo ya watu ni Tshishimbi wa Yanga na Danny Usengimana wa Singida United,Emmanuel Okwi wa Simba