Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 6:42 am

MAKALA : NI VITA YA ARSENAL NA CHELSEA LEO UWANJA WA EMIRATES

ARSENAL VS CHELSEA SAA 4.45 USIKU

Moja kati ya michezo inayo tikisa jiji la London lenye watu takribani milioni 8.7 kwa takwimu za mwaka 2016 basi ni mchezo kati ya Arsena anapo kutana na Chelsea kutokana na ushindani na ukubwa wa mashabiki walio nao mahasimu hawa wawili katika jiji hilo ndani ya miaka ya hivi karibuni.

Mvuto wa mechi hizi unachagizwa sana na ubora wa wachezaji wanao kipiga katika klabu hizi huku pia zikiwa ni timu ambazo kwa takriba miaka 15 zimekuwa zikivutana kusalia katika nafasi nne za juu na pengine kuchukua ubingwa kabisa.

NINI KILI SABABISHA UHASIMU WAO?NGOJA NIKURUDISHE MBALI KIDOGO KATIKA HISTORIA

Kabla ya mwanzoni mwa miaka ya 2000(2000c)klabu hizi mbili hazikuwa na mvutano mkubwa sana pale ambapo zimekuwa ziki kutana kutokana na ukweli kwamba hapo awali klabu ya Chelsea haikuwa ikifanya vizuri sana na kuhesabiwa kama moja kati ya timu zenye nguvu katika Ligi kuu ya Uingereza.

Baada ya kuja uwekezaji wa Mrusi Roman Abramovich kuliifanya Chelsea kujikita zaidi katika mbio za ubingwa kwa upande wa nyumbani(domestically) EPL,FA CUP,CARLING CUP (CAPITAL CUP NA BAADAYE CARABAO CUP) na hata ile ya nje ya mipaka ya Uingereza kama UEFA Champions League na hata EUROPA League.

Mrusi huyo haku sita kuleta majina makubwa kaita kikosi chake ili kuhakikisha anakifanya kuwa bora zaidi na hata kuleta waalimu wenye uwezo mkubwa na majina ya kutisha ndani ya kikosi cha Chelsea,hapa ndipo walimu kama Jose Mourinho ,Carlo Ancelotti na wengine wengi mpaka kocha wao wa sasa Antonio Conte wote wamekuja Chelsea wakiwa tayari wamefanya makubwa na vilabu vingine.

Japo kuwa hapo awali hakukuwa na ushindani ama uhasimu mkubwa kama ulivyo hivi sana lakini bado mechi baina ya timu hizi ulikuwa unaleta msisimko kwa mashabiki wengi kushuhudia kama ilivyo tia fola mwaka 1907 ikiwa ni miaka miwili tangu klabu ya Chelsea kuundwa mwaka 1905 mchezo ukiwa darajani Stamford Bridge mshabiki walikadiriwa kufika 65,000 na hata hivyo haikuiishia hapo bado klabu hizo zilipo kutana kuliendea kuwa na namba kubwa ya watu walio jitokeza kutazama michezo yao huku pia umaarufu wa jiji la London kwa kupokea wageni mbali mbali kutoka nje na ndani ya nchi ukichagiza idadi ya watazamaji wa michezo hiyo.

Usajili wa beki wa kushoto wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Ashley Cole kutoka Arsenal kwenda Chelsea mwka 2006 pia unatajwa kuchagiza uhasimu mkubwa,kwanza ulianzia kwa mashabiki wa Arsenal wakimshutumu mchezaji huyo kuwa mpenda pesa kitu kilicho pelekea hata kumzomea kwenye baadhi ya michezo yake ya awali,

kisha ukahamia hata kwa wachezaji kama utakuwa na kumbukumbu nzuri mwaka 2007 katika mchezo wa kombe la Ligi ulio zikutanisha timu hizi mbili ulikuwa ni mchezo uliokuwa na maseke ya kutosha kwanza ukianzia kwa Frank Lampard, Cesc Fabregas ambao hawa kwa pamoja walikula kadi za njano kutoka kwa mwamuzi bora kwa wakati huo huku wachezaji watatu John Obi Mikel,Kolo Toure na Emannuel Adebayo wakipatiwa umeme,mchezo ukiisha kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

REKODI ZA MAHASIMU HAO WAWILI

Kwa ujumla timu hizi zimekutana mara 171 huku Arsenal akiibuka na ushindi mara 64 na Chelsea mara 57 sare ni 50,mfungasji bora wa muda wote katika michezo inayozikutanisha timu hizi ni Didier Drogba aliye pachika mabao 13.

Magoli mengi kabisa yalio wahi kufungwa katika mechi zinazo wakutanisha mahasimu hawa ni 6,

Chelsea 1-5 Arsenal (1930-31)

Chelsea 6-0 Arsenal (2013/14)

KATIKA MCHEZO WA LEO

Katika mchezo wa leo timu hizi zinakwenda kukutana huku zikiwa na tofauti ya point saba yani Chelsea yuko nafasi ya pili akiwa na alama 45 na Arsenal yuko nafasi ya 6 akiwa na alama 38.

ARSENAL

Arsenal imekuwa unpredictable(isiyotabirika)msimu huu kutokana na kuwa na form ya kushuka na kupanda katika kila mchezo,lakini pia imekuwa ikibadili mbinu kulingana na kila mchezo.

Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri klabu ya Arsenal ilianza msimu ikiutumia mfumo wa 3-4-3 lakini katiaka mechi za hivi karibuni imejaribu kurudi katika mfumu wake wa awali wa 4-3-3 unao toa fulsa kwa Ozili na Sanchez kwenda wide kuingia na kutoka katika box la mpinzani.

Wakati mwingi klabu ya Arsenali imekuwa ikinufaika na uwepo wa mshambuliji Alexandre Lacazette kutokana na uhodari wake wa kupachika mabao,kasi na uwezo wa kupambana akishirikiana na viungo wengine washambuliaji kuhakikisha wanalisakama sana lango la wapinza kwa dakika 90 za mchezo.

Maeneo muhimu kwa Arsenal hii leo ni eneo la katikati ambako kwa misimu mingi sana mzee Arsene Wenger amekuwa kilitumia kama nguzo yake kuhakikisha anapata matokeo japo kwa miaka ya hivi karibu amekuwa kitumia hata mabeki wake wa pembeni kupunguza majukumu ya ma wingi wake nyakati za kushambulia,urejeo wa Jack Wilshere ndani ya kikosi unaleta rithim ya tofauti sana na taratibu anaanza kuifanya timu kutengeneza momentum ya kuvutia nyakati zote za kushambulia na kukaba pia.

Hata hiyo klabu hiyo ndani ya msimu huu imepata matatizo makubwa sana katika nafasi yake ya beki wa kati na hapa Arsene Wenger amejitahidi sana kufukia mashimo kwa kujaribu kutengeneza ukuta wa watu 3 katika mfumo wa 3-4-3 bado kumekuwa na tatizo,nafikiri hii ndio sehemu ambayo Chelsea kama wataitumia vilivyo wataiadhibia Arsenal.

CHELSEA

Mwalimu Antonio Conte anafahamu kwa uzuri umuhimu wa mchezo huu hasa kutokana na nyakati timu yake ilipo kwa sasa na hata presha anayoipata kutoka wa Manchester City katika mbio za ubingwa.

Msingi wa Chelsea bado utaendelea kutegemea ubora kiungo Ng’olo Kate na hii kutokana na uwezo wake wa kuzuia mashambulizi na kuwalinda mabeki watatu wanaunda ukuta wa Chelsea

Bado Chelsea iataendelea kutumia mfumo wa mabeki watatu japo namuona Antonio conte akibadili kidogo structure ya mbele kwa kuweka viungo wa tano na washambuliaji 2 na hii ni kutokana na amkutana na waandishi wa habari alioweka wazi kuwa katika michezo dhidi ya timu kubwa atatumia viungo watano kuhakikisha anapunga makali ya timu pinzani.

Matokeo ya Chelsea yanategemea ubora wa miguu ya nyota wao Eden Hazard ambaye tangu kujiunga na kikosi hicho amakuwa mchezaji muhimu na maetoa msaada mkubwa sana ,kwamsimu huu katika michezo 26 amefunga magoli nane na kusaidia upatikana wa magoli mengine nane.

Sehemu pekee dhaifu kwa Chelsea ambayo itakuwa na mwanya wa kuwafanya Arseanal kutoka kifua mbele kama watatumia ni sehemu ya upande wa kushoto anakocheza Marcos Alonso ambaye amaekuwa mchezaji muhimu sana hasa timu ikiwa inashambulia na kutokana na uwezo wake mzuri wa upachikaji mabao lakini mapungufu makubwa katika kukaba.

Kwa ujumla mchezo hautakuwa rahisi sana japo kuwa Chelsea anapewa nafasi ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo