Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:02 pm

LUGOLA: MWANANCHI ANAWEZA KUFA HATA AKIWA ANAFANYA MAPENZI

Dodoma: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema kuwa wananchi kufia kwenye vituo vya polisi haina maana kwamba ameteswa kwa sababu mwananchi huyo anaweza pia kufia kwenye maeneo mengine kama vile bungeni, kwenye gari, hata akiwa anafanya mapenzi kifo kinaweza kumtokea.

Related image

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 13 Bungeni Dodoma baada ya kuulizwa swali la nyongeza na Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF) ambaye alitaka ufafanuzi kwamba Katika siku za hivi karibuni kumetokea tabia mbaya na chafu na ovu kabisa ya Mahabusu kufia kwenye vituo vya Polisi. Mahabusu wanapelekwa wanapata mateso yanayopelekea vifo vyao, kuna baadhi ya jamii zimekataa kuchukua maiti kwenda kuzizika

Lugola akajibu "Mwananchi kufa, anakufa wakati wowote na mahali popote . Sijui kwenye Quran lakini kwenye Biblia ukisoma Muhubiri 9:12 kifo ni mtego, kifo humnasa mtu wakati wowote na mahali popote"


"Mtu anaweza kufa akiwa polisi, akiwa anafanya mapenzi, anaweza akafa akiwa kwenye gari anasafiri na aweza kufia hata humu Bungeni kwahiyo isije ikachukuliwa kwamba nayefika kituo cha polisi ni kwamba ameteswa"

"Lakini nikiri kuwa kuna matukio ya Watu kufia mikononi mwa Polisi, na pale ambapo matukio hayo yanajitokeza huwa tunafanya uchunguzi na ikibainika Polisi wanahusika huwa tunachukua hatua" amesema Lugola

Aidha Lugola amesema Ndio maana tunawazuia wananchi wasichukue sheria mkononi na kwenda kuchoma kituo cha polisi. Mbona huyu anayefia akifanya mapenzi mbona hawaendi kuchoma kitanda?