- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
LUGOLA ATAKA DHAMANA KUTOLEWA SIKU ZOTE ZA WIKI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Polisi wote nchini kutoa dhamana kwa watuhumiwa kwa siku zote za wiki zikiwemo Jumamosi na Jumapili.
amesema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 katika siku zote za wiki na si vinginevyo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwamo siku za mapumziko.
“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi Ijumaa ikifika Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana hadi Jumatatu, hii tabia si sahihi na ife haraka iwezekananavyo,” amesema Lugola.
Lugola amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, na uongeza kuwa ni marufuku kwa askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.
Pia Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari Polisi kutoza fedha kwa ajili ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini.