- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
LOWASSA: MOTO WA CHADEMA UCHAGUZI 2020 HAUZIMIKI
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ameonesha kukasirishwa na hama hama ya wapinzani kuelekea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maneno hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Monduli, Julias Kalanga (Chadema). Kalaga kuhamia CCM usiku wa kuamkia Julai 31, 2018.
Hata hivyo Lowassa amesema, umahiri wa Chadema na moto wake kwenye Uchaguzi Mkuu ujao hauzimwi.
Lowasa kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ameeleza kuwa, CCM imebadili mbinu na kuamua kurubuni wabunge na madiwani wa upinzani kutokana na ‘moto’ wa upinzani uliowashwa mwaka 2015 kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.
“Moto ule tuliouwasha 2015 hauwezi hata mara moja kuzimwa na mbinu hizi. Wataondoka kina Kalanga wengi tu lakini kasi ya moto ule jinsi ilivyo sasa ndani ya mioyo ya Watanzania ni ya moto wa kiangazi,” amesema Lowassa na kuongeza;
“Kalanga hakuwa na sababu za msingi za kujiuzulu nafasi yake hiyo ya heshima ya kuwatumikia wananchi wa Monduli nikiwemo mimi. Uamuzi huo umetuhuzunisha na kutuumiza.
“Lakini nawaomba msife moyo hata dakika moja zaidi, kitendo hicho cha Kalanga kizidi kutupa nguvu, ari, hamasa na mori zaidi wa kuendeleza mapambano ya kuitafuta demokrasia na mabadiliko ya kweli.”
Amesema kuwa, kuhama kwenye siasa sio tukio jipya kwenye dunia hivyo sio sababu ya kurudi nyuma kwenye mapambano, “hakuna jipya katika hili, ni kawaida kwa wana siasa duniani kuhama vyama vyao na kubadilishana vijiti.”
Lowassa alihama kutoka CCM na kujiunga Chadema mwaka 2015 kisha kupewa nafasi ya kukiwakilicha chama hicho kama mgombea urais ambapo aliungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Vyama vinavyounda UKAWA ni pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha NCCR-Mageuzi, NLD na Chadema.