- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
IRAN IMESEMA IKOTAYARI KUHARIBU MALI ZA RAIS TRUMP
Kamanda mmoja wa Kikosi cha kijeshi nchini Iran amemuonya vikali rais wa Marekani Bw. Donald Trump kwamba taifa lake likotayari kuharibu 'kila kitu kinachomilikiwa na rais huyo' iwapo Marekani itathubutu kuishambulia Iran.
Meja Jenerali Qassem Soleimani aliapa kwamba iwapo bwana Trump ataanzisha vita, 'jamhuri ya Iran itamaliza vita hivyo.
Matamshi yake yanafuatia matamshi ya Trump katika mtandao wa Twitter akimuonya rais wa Iran kutojaribu kutishia Marekani.
Hali ya wasiwasi imezuka tangu Marekani ilipojiondoa katika makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ya mwaka 2015.
Meja jenerali Soleimani-ambaye anaongoza kitengo cha jeshi la Quds kutoka katika jeshi la Iran la elite Revolutionary Guards - alinukuliwa siku ya Alhamisi akisema, 'kama mwanajeshi ni wajibu wangu kujibu vitisho vyako'.
"Zungumza nami sio rais [Hassan Rouhani]. Sio heshima ya rais wetu kukujibu''
"Tunakukaribia , pale ambapo huwezi dhania. Njoo tuko tayari''.
"Iwapo utaanza vita, tutamaliza vita hivyo. Unajua kwamba vita hivi vitaharibu kila unachomiliki."
Pia alimshutumu rais huyo wa Marekani kwa kutumia lugha ya vilabu vya burudani na maeneo ya kucheza kamare".
Siku ya Jumapili, bwana Trump alituma ujumbe wa kumtishia rais wa Iran.