Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:42 pm

HABARI 6 ZILIZOJIRI BUNGENI LEO NI PAMOJA NA FAINI YA UCHANGUDOA NI MIA 500 AU 1000

Zifuatazo ni habari 6 kubwa zilizobamba leo Jijini Dodoma Bungeni

1. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kuwa serekali imekuwa ikipambana na changamoto katika kutekeleza sheria ya adhabu kwa wanawake au wanaume wanaofanya biashara ya kujiuza maarufu kama changudoa hapa nchini.

Image result for Machangudo

Masauni ameyasema hayo leo September 14 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali kuwa ni namna gani Serikali imejipanga kutokomeza biashara hiyo ya ngono. Amesema Serikali inajitahidi kuhakikisha inatokomeza biashara ya 'uchangudoa' ingawa inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za sheria

Image result for Machangudo


Mfano, Kanuni ya adhabu namba 176(a), sura ya 16 inasema adhabu inayotakiwa kutolewe kwa wanaofanya biashara ya 'madanguro' ni faini ya Tsh. 500 au Tsh. 1,000 ikiwa ni kwa mara ya pili au zaidi

Aidha, Naibu Waziri ameliomba Bunge kuwa ni wakati sasa wa sheria hizo kufanyiwa mabadiliko kwani kwa kiasi fulani zinachochea kuendelea kuwepo kwa biashara hizo

2. ''Uchunguzi wa kesi ya kushambuliwa kwa Tundu Lissu, tumekuwa tukihitaji kupata ushirikiano kutoka kwa chama anachotoka (CHADEMA), akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha lakini wao wamekuwa wakijitahidi kumficha hivyo kuchelewesha uchunguzi''

Naibu waziri huyo ameyasema hayo leo Bungeni.


Mengineyo yaliyojiri Bungeni leo ni;

3. Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema, mikoa yote nchini ina sukari ya kutosha na kwamba, kuendelea kuisambaza zaidi haitapunguza bei ya bidhaa hiyo.

4. Serikali kupitia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi imekanusha taarifa zinazolishutumu Jeshi la Uganda kuwapiga wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani nchini Congo.

'Hakuna ukweli kwamba majeshi ya Uganda yanashiriki kuwapiga askari wa Tanzania walioko nchini DR Congo kwenye shughuli za kulinda amani. Tuna uhakika ni vikundi vya waasi''

Tathmini ilifanyika mwezi June mwaka huu, inaonyesha kwamba uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu huu wa 2017/18 ni tani Milioni 16.9".Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

5. Serikali inaendelea kumtangaza kama kivutio cha utalii samaki aina ya Papa Potwe anayepatikana maeneo machache sana duniani huku Tanzania akipatikana katika visiwa vya Mafia na Zanzibar. Samaki huyo mara nyingi hufikia uzito wa tani 20 na urefu wa mita 8'' - Mgimwa

6. Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Bunge la 11 ndiyo lenye wasomi wengi kuliko mabunge yote yaliyopita, ametaja idadi ya wenye shahada za Uzamivu PhD ni 29 kati ya hizo 27 zinamilikiwa na wabunge wa CCM, moja CHADEMA na moja mbunge wa CUF

Serikali imelieleza Bunge kuwa, si kweli kwamba Mwenge wa Uhuru unatumia fedha nyingi za walipa kodi na haioni umuhimu wa kuuweka Makumbusho ya Taifa.