Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:48 am

GOOD NEWS KWA WATUMIAJI WA TWITTER YAONGEZA MANENO MPAKA 280

Marekani: Mtandao wa Twitter umeanza kuongeza maneno ya kuweka kwenye ujumbe wakati wa kuposti, watumiaji wake wataweza kuandika ujumbe kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140 yaliyo kuwepo awali.

Hapo awali Septemba mwaka huu Kampuni hiyo ilikuwa imewawezesha baadhi ya watu kutumia tarakimu hizo lakini kwa majaribio.

Wakati wa majaribio, ni ujumbe kwa asilimia 5% ambao ulikuwa na urefu wa zaidi ya tarakimu 140 na ni asilimia 2% uliokuwa na zaidi ya tarakimu 190, wamesema twitter

Lakini walioandika ujumbe mrefu walipata wafuasi zaidi, walihusiana na watu zaidi na walitumia muda zaidi katika mtandao huo.

"Tuliona kwamba watu walipohitaji zaidi ya tarakimu 140, waliandika ujumbe kwa urahisi na mara nyingi. Muhimu zaidi, watu waliandika ujumbe wa chini ya tarakimu 140 mara nyingi zaidi na ufupi wa ujumbe wa Twitter ulisalia," meneja wa bidhaa na huduma wa Twitter Aliza Rosen ameandika.

Mabadiliko hayo yalipotangazwa mara ya kwanza, wengi waliyakosoa na kusema badala yake wangelipenda kuona taarifa za chuki pamoja na mashine zinazoandika ujumbe zikidhibitiwa zaidi.

Aidha, wengi walitaka ujumbe urudi kufuata historia tena, ujumbe wa karibuni zaidi ukionekana mwanzo na pia waweze kuhariri ujumbe.

Mtandao huo kwa sasa una watu 330 milioni, idadi ambayo ni ya chini ukilinganisha na 800 milioni wa Instagram na zaidi ya 2 bilioni wa Facebook.