Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:44 am

GODBLESS LEMA: KUTEKWA KWA MODEWJI KUTASHUSHA UCHUMI WA NCHI

Dar es Salaam: Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amesema kuwa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ litasababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchini.

Lema ambaye pia ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, ameongeza kuwa kulingana na tukio hilo wawekezaji watakuwa na hofu ya kuendelea kuwekeza hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 16, 2018 Lema amesema tukio hilo na mengine yaliyokwisha tokea yanazua hofu miongoni mwa wawekezaji ambao huenda wakakimbilia nchi jirani.

“Watu wenye capital (mitaji) wataondoa mitaji yao watakwenda nchi zenye usalama. Watu wataogopa watoto wataanza kutekwa, familia zitaanza kusumbuliwa na kwa sababu haya matukio yamekuwa ni mfululizo,” amedai Lema.

Lema amesema mbali na familia ya Dewji kutangaza dau kwa atakayesaidia uchunguzi wa tukio hilo bado familia ina uwezo wa kuajiri wapelelezi binafsi wa kimataifa huku akiitaka Serikali kuruhusu wapelelezi binafsi.