Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:46 am

FATMA KARUME: KULIKOSOA JESHI LA POLISI NI HAKI YETU YA MSINGI

Dar es salaam: Rais wa Chama cha mawakili Tanzania (TLS) Fatma Karume amelitaka Jeshi la Polisi nchini Kufanya kazi yao kwa uwadilifu ili wananchi wawe na imani na Jeshi hilo.

Akiongea Leo Octoba 20, 2018 Fatma ambaye ni mtoto wa kike wa aliyekuwa muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Rais Abeid Karume amesema kuwa hakuna mwananchi anapenda kuwa Adui wa Jeshi hilo huku akisisitiza kuwa wananchi kulikosoa jeshi hilo ni haki yao ya Kimsingi.

"Nimepata huzuni sana na maneno ya IGP kwenye Press Conference yake. Hakuna mtu anataka UADUI na Polisi. Tunataka Polisi wafanya kazi yao ili sisi kama wananchi tuwe na imani nao na tuishi kwa salama"

"Kulikosoa jeshi la Polisi ni HAKI yetu ya msingi na kamwe hatutoliogopa polisi" aliandika Fatma kupitia ukurasa wake wa twittwer.

Kauli ya Fatma imekuja mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro kusema leo kuwa watu wanatengeneza uwadui na jeshi la Polisi huku wakikosoa usiku kucha kazi inayofanywa na Jeshi hilo

Kauli hiyo ya Sirro ameitoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari kuelezea juhudi zilizofanikisha kumpata Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji leo Octoba 20. 2018

“Lakini mtu kupitia Social media amelala na mke wake anapata kiyoyozi anachallenge kazi zote za Polisi”

“Na najiuliza unapojenga uadui na majeshi yako unatumwa na nani? Ili iwe nini” alisema Sirro.

Dewji alitekwa siku ya Alhamisi ya Octoba 11, 2018 Katika Hoteli ya Calliseum iliopo Jijini Dar es salaam akiwa katika mazozei ya viungo.