Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:45 am

FATMA KARUME :KAZI YA POLISI SIO KUKAMATA TU PIA KUTOA DHAMANA

Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) Fatma Abeid Karume maarufu kama Shangazi amesema kuwa Polisi wana wajibu wa kuwapa watu dhamana, na iwapo watalazimika kuendelea kumshikilia mtuhumiwa wanatakiwa kuongeza masaa 8, na iwapo itahitajika zaidi ni lazima polisi hao wapate kibali kutoka mahakamani

Akiongea Leo Oct. 2 2018 kupitia Kituo cha habari cha East Africa Redio Fatma amesema kuwa polisi wanawajibika kutoa dhamana siku zote za wiki hata siku za week end kama jumamosi na jumapili.

"Suala la polisi kutoa dhamana Jumamosi na Jumapili, ni wajibu wao, kama wanafanya kazi siku hizo na wanalipwa, kazi yao sio kukamata tu, bali hata kuwaachia kwa siku hizo". Amesema Fatma

Aidha Fatma amesema Chini ya sheria za hapa nchini, dhamana sio lazima mtu atoe pesa, kuna conditions za dhamana kama tano tofauti, ikiwemo dhamana inaweza kuwa inaandikwa tu kwa maandishi unakubali kwamba utakwenda mahakamani siku ukiitwa,

"Pili unaweza kukubali tunakutoa kwa dhamana tunaendelea na upelelezi, au unaweza ukamleta mama yako, akasema mimi ni mama wa Juma namdhamini na nitakahikisha anakuja mahakamani"

"Ya mwisho ndiyo pesa, unaweza ukatoa pesa kama dhamana, siku ukipelekwa mahakamani, unatoka kwenye mikono ya polisi, unatakiwa urudishiwe pesa yako" alimalizia Fatma

Kauli hii fatma imekuja siku chache baada Waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola kupiga marufuku watuhumiwa kuwekwa mahabusu bila kupewa dhamana kwa kisingizio cha muda wa kazi kuisha.

Aidha lugola aliwataka Polisi wote kutoa dhamana kwa watuhumiwa siku zote za wiki mpaka week ends