- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: RAPA KANYE WEST ABADILISHA JINA NAKUITWA 'YE'
U.S: Rapa mkali wa miondoko ya Hip Hop nchini Marekani Kanye West ameamua kubadilisha jina lake muda mrefu na kuitwa "Ye"
Akitoa mabadiliko hayo kwenye ukurusa wake wa Twitter jana siku ya Jumamosi, aliandika: "Nimekuwa nikijulikana kama Kanye West. Mimi ni YE."
Kanye alisema kwamba "Ninaamini 'ye' ni jina linatumika sana kwenye Biblia na kwenye Biblia linamaanisha 'wewe,'" West alisema mapema mwaka huu wakati akizungumzia albamu yake na mtangazaji wa redio Big Boy.
"Kwa hivyo mimi ni wewe, mimi ni sisi, ni sisi. Albamu hii ni ishara ya vile tulivyo."
Kanye mwenye umri wa , 41, amekuwa akiitwa Ye kwa muda na kulitumia jina hilo kama kichwa cha albamu yake ya nane ambayo ilitolewa mwezi Juni.
Mabadiliko hayo yalikuja kabla ya tamasha moja wa siku ya Jumamosi ambapo alitarajiwa kuzindua albamu yake mpya ya Yandhi.
Ni mmoja wa marapa kadhaa waliobadilisha majina yao.
Sean Combs awali alikuwa akijulikana kama Puff Daddy, P. Diddy au Diddy lakini mwaka huu alitangaza majina ya Love na Brother Love.