Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:50 am

BURUDANI : NDOA YA SHISHI BABY HAINA MWALIKO,NI NAULI YAKO TU

Ndoa isiyokuwa na Mwaliko haina uchoyo kabisa fanya tu kujiandaa! ni nauli yako tu

Mwimbaji na Mwigizaji wa Bongo Mwanadada Zuwena Mohamed au ‘ Shilole’ amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa yake Desemba, mwaka huu na mpenzi wake Ashirafu Uchebe, lakini sherehe hiyo haina kadi wala mwaliko maana itafanyika Open space-sehemu ya wazi

Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ akiwa na mpenzi wake

Shilole amesema anamshukuru Mungu, mpenzi wake huyo ameshatoa mahari kubwa nyumbani kwao, kwa hiyo kilichobaki sasa hivi ni ndoa tu na haitakuwa ya kuhudhuriwa na watu maalumu kama wanavyofanya wengine, bali kila mmoja anaweza kuishuhudia.

“Ndoa yangu sitafanya ya siri kama wanavyofanya watu wengine, nitafanya sehemu ya wazi kabisa na wala haitakuwa na kiingilio hata kidogo, maana napenda ionwe na watu wote na washuhudie kila kinachoendelea,” alisema Shilole.