Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:24 pm

BURUDANI : MKALIWENU - AFUNGUKA MAISHA YAKE YA SASA BAADA YA KUONDOKA TIMAMU

Nawalipa Mwenyewe Camera Man na Wote wanaofanya ukaona Videos zangu Youtube na Instagram-Mkaliwenu

Mchekeshaji Jackson Supakila,maarufu kwa jina la mkaliwenu kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake ya sasa,tofauti na alivyokuwa kwenye kampuni ya Timamu media Group

Mkaliwenu ambaye miezi kadhaa nyuma alihama kwenye kampuni ya Timamu Media Group ameeleza kuwa maisha yake kwasasa yamekuwa ya kujitegemea mwenyewe kwa kila kitu katika kuendeleza kazi yake ya kuchekesha

Ameeleza kuwa kwasasa anafanya kazi pekeyake bila uongozi,hali inayomlazimu kila kitu kinachopeleka mbele kazi yake basi anatoa pesa yake mwenyewe,kuanzia watu wa kamera na wote wanaofanya mchekeshaji huyo kuendelea kufanya kazi kwa wakati huu

"Tangu nitoke timamu maisha yamebadilika kidogo sasa ivi nafanya kazi kwa kujitegemea kila kitu,pesa yangu ndio nalipa kila kitu kuhakikisha kazi zangu zinaenda"anasema mkaliwenu

Pia ameeleza kuwa mitandao ya kijamii aliyokuwa akitumia wakati yupo Timamu sio kwamba alinyang'anywa kama watu wanavyodai bali aliamua mwenyewe kuiacha,kwa amani bila tatizo lolote

Mchekeshaji huyo pia amesema hajawahi kufikilia hata siku moja kama anaweza kurejea Timamu Media Group,kwasababu ameridhika na anachokifanya kwasasa ingawaje kuna changamoto nyingi lakini anajaribu kufanya vitu tofauti ili aweze kusonga mbele


Uhusiano wake na wachekeshaji wenzie,Ebitoke, Mjeshi na Mama Ashura amesema kuwa ni kama mtu na mpenzi wake wakiwa pamoja na kuachana

"Uhusiano wangu na Ebitoke,Mama Ashura na Bwana Mjeshi ni kama mtu alikuwa na mpenzi wake wakaachana hivyo tu"anafunguka Mkaliwenu

Mchekeshaji huyo ambaye alianza kujinyakulia umarufu akiwa Timamu Media Group pia amedai anauwezo mkubwa wa kuimba miziki yote Rnb Taarabu na Hiphop.