- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : LADY JAY DEE AFUNGUKA KWANINI HATOI BACK TO BACK
Mwanamuziki mkongwe kwenye muziki wa Bongo fleva Lady Jay Dee amefunguka na kueleza sababu zinazomfanya ashindwe kutoa nyimbo mara kwa mara
Lady Jay Dee amesema wale wanaotoa nyimbo mfululizo huenda kuna faida wanayoipata kwa kufanya hivyo,lakini ni tofauti na kwake, kwani sio utaratibu ambao amejiwekea kutoa nyimbo mara kwa mara katika kazi zake za muziki
“Mimi huwa sitoi ngoma hivyo, huwa sitoi ngoma kila siku, kwa hiyo kwa wanatoa ngoma kila siku wanazo sababu zao, wanaweza wakaelezea pengine inaweza ikawa na manufaa kwao,”alisema Lady Jay Dee
Muimbaji huyo wa muda mrefu kwenye muziki kwa kipindi cha muda mrefu alikuwa kimya katika muziki kabla ya kurejea upya na ngoma ambayo kwa sasa inatamba katika baadhi ya vyombo vya habari
Tangu atoe wimbo wa Baby" alikaa kimya takribani miezi mitatu kabla ya kurejea na wimbo wa I miss you ambao unaendelea kufanya vizuri kwenye radio tofauti
Kwasasa msanii huyo anafanya vyema na wimbo wake wa I miss you,ambapo mpaka sasa hajaweka wazi siku ya kutoa ngoma yake nyingine baada ya I miss you