Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 8:38 am

BURUDANI : GHARAMA ZA HARUSI YA MWANAMFALME NI NI KUFURU SI MCHEZO KABISA

Jumamosi iliyopita ilishuhudiwa sherehe kubwa ya harusi iliyoteka dunia kwa muda iliyokuwa inamuhusu Prince Harry na mpenzi wake wa muda mrefu Meghan Markle.

Ndoa hiyo ilihudhuriwa na wageni zaidi ya 4000 kutoka mataifa mbali mbali duniani huku mastaa wakubwa duniani kama David Beckham, Oprah Winfrey, Priyanka Chopra, Serena Williams na wengine wakiwa miongoni mwa walioalikwa.

Je unafahamu gharama zilizotumika kuandaa shughuli hiyo? Basi ndoa hiyo inaweza ikaingia kwenye kitabu cha rekodi kuwa miongoni mwa ndoa zilizotumia gharama kubwa dunia.

Kwa mujibu wa Bridebook ambao wanashughulika na masuala ya harusi na Sherehe, umeripoti kuwa ndoa hiyo imegharimu kiasi cha paundi milioni 34 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 103 za Kitanzania.

Lakini pia ndoa hiyo imeweza kuzidi gharama za ndoa ya Prince William (Duke of Cambridge) na mkewe Catherine Middleton iliyofungwa April 2011 ambayo inadaiwa kuwa ilitumia kiasi cha paundi milioni 32.

Gharama za gauni alilovaa Meghan Markle ambalo limebuniwa na Claire Waight Keller limetajwa kugharimu kiasi cha paundi 300,000. Gharama ya gauni hilo limeweza kuizidi gauni la Cate Middleton alilovaa kwenye ndoa yake na Prince William ambalo liligharimu kiasi cha paundi 250,000 lililobuniwa na Alexander McQueen.

Hizi ni baadhi ya gharama nyingine za harusi ya Prince Harry na Meghan Markle:

Keki – £50,000
Muziki – £300,000
Mapambo – £130,000
Pete za ndoa – £6,000
Kupamba nywele na Makeup – £10,000
Gharama za fungate (Honey Moon) – £120,000
Vinywaji – £193,000
Chakula – £286,000
Gharama za ukumbi – £350,000