- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : EBITOKE AKIRI PENZI LAKE NA BEN PAUL KUIMARIKA UPYA
Mchekeshaji kutoka kikundi cha Timamu,Ebitoke amefunguka kwa mara nyingine kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na msanii mwenzake wa muziki wa bongo fleva Bernad Paul maarufu kama Ben Paul
Kupitia mahojiano maalumu mchekeshaji huyo amesema licha ya kuwa na migogoro na na mwenzake huyo lakini kwa sasa mapenzi yao yanaendelea kama kawaida na hakuna tatizo tena kwenye mahusiano hayo
mara kadhaa ebitoke alikuwa akidai Ben paul hapokei wala kujibu ujumbe aliokuwa akimtumia kwa njia ya simu hali iliyowacha watu midomo wazi na kuhisi huenda penzi lao lingekuwa limekwisha
“Hapana sijaachana naye, baada ya kulalamika kuwa hapokei simu yangu sasa hivi tupo vizuri kabisa, mlikuwa mnatuona hata kwenye baadhi ya show zake tupo pamoja, sasa hivi tupo fresh yeye ndiye boyfriend wangu sina mwingine,” alisema Ebitoke.
Uhusiano wao umekuwa ukiyumbayumba huku kukiwa na sintofahamu nyingi, kwani ebitoke amekuwa ni mtu wa kulalamika kwenye mitandao na vyombo vya habari kila anapoona mwenza wake anakwenda tofauti na matarajio yake
Uhusiano wa Ebitoke na Ben Paul ulianza Juni mwaka huu mara baada ya Ebitoke kujitokeza katika mitandao na vyombo vya habari na kudai kuwa anavutiwa na Ben Paul na angetamani kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi kitu ambacho kinaelezwa kilikuja kutimia hapo baadaye.