Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:41 pm

BURUDANI: DIAMOND AWATAKA WASANII KUWA NA MSIMAMO KWENYE MALIPO

Msanii nyota wa Muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul Maarufu kama DiamondPlatnumz amewataka wasanii wenzake wa Muziki kuamka kwenye swala linalohusu malipo wakati wa Majadiliano ya Kufanya Show.

Diamond amewataka wasanii hao kutaja kiasi cha Fedha kitakachokuwa na thamani sawa na muziki wanaoufanya ambacho kitakachomfanya kuishi yeye na Familia yake.

"Haya sasa wasanii kazi ni kwenu kuhakikisha unamsimamo na hata unapotakiwa unataja dau litalowezesha kusaidia familia yako kesho na keshokutwa...sio tena kujipeleka halafu kesho kuleta malalamiko eti ooh umenyonywa! utakuwa ni ujinga wako.. sie tushaanza kumaliza kazi!!" Aliongea Diamond kupitia ukurasa wake wa twitter

Diamond amesema kwasasa wasanii wanathamani na hata wale waliokuwa wanasema hawauzi wanaanza kupewa pesa ya kufanya show.

"Adabu imewakaa sasa, wanaanza kuwaheshimu na kuwakumbatia wasanii...Hata wale walosema hawauzi sasa wanawaona wanathamani...Eti hadi kucheza nao kikapu...... na hii ndio Maana halisi ya Mapinduzi ya Burudani!! yani Tuheshimiane" alisema Diamond

Diamond kwasasa yupo mkoani Mtwara kwenye show ya Wasafi Festival2018 inayotarajiwa kutimua vumbi tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu.