- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : BARAKA THE PRINCE AFUNGUKA KUVURUNDA MWAKA 2017
Barakah The Prince aeleza kilichomfanya avurunde
Msanii wa muziki, Baraka The Prince amefunguka kueleza kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri kimuziki mwaka 2017.
Muimbaji huyo ambaye mwaka 2017 aliachana na label ya Rock Star4000 na kuanzisha label yake, Bana Music, amedai sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vizuri ni kukataa baadhi ya show ambazo alikuwa anapewa na mapromota.
“Mi nimiongoni mwa wasanii ambao nabagua sana show, mpaka nikifanya show mpaka promota afike bando ambalo nahitaji, na ninafaya hivyo ili kulinda brand yangu ambayo tayari nimeshaitengeneza,” Baraka alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Aliongeza,”Na kama nimeyumba kimaisha nayumba kweli kwa sababu maisha ndivyo yalivyo, kuna kupanda na kushuka, mpaka mataifa mkubwa wanayumba kiuchumi mimi ni nani, sio kitu kibaya, kinaweza kumtokea mtu yeyote”,
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa maashabiki kuwa msanii huyo sio tu amefulia, bali hata uwezo wake kwenye kazi umeshuka, na kushauri kama inawezekana awe anaandikiwa kazi zake.