- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: ALICHOKIONGEA MASANJA BAADA YA DIAMOND KUZUILIWA NA BASATA
Dar es salaam: Muigizaji maarufu wa comedy nchi Tanzania Emmanuel Mgaya maarufu kama MASANJA ameoneshwa kusikitishiswa na Baadhi ya Watanzania wanaofurahia mtu kupata tatizo kwa sababu tu ya mafanikio yake na juhudi zake na kusema Kuwa tabia kama hiyo inahitaji maombi ya kitaifa.
Masanja ameyasema hayo leo Mchana baada ya Baraza La Sanaa La Taifa Tanzania (BASATA) Jana kumzuia mwanamuziki wa Africa Mashariki Diamond Platnumz katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam kwenda nchini Madagascar kwa show.
"Diamond ni mmoja ya vijana wanaojituma kufanikiwa na kusaidia watu wengi kufanikiwa. Huwezi kupendwa na kila mtu lakini hii sumu ya baadhi ya Watanzania kufurahia mtu akipata tatizo au kumzushia upopompo anapofanikiwa au kuchukia mtu kupiga hatua inahitaji maombi ya Kitaifa." aliandika Masanja kupitia ukurasa wake wa twitter.
Jana asubuhi Diamond alilazimika kusubiri kwa saa tisa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kutokuwa na kibali hicho cha (Basata).
Mwanamuziki huyo wa IYENA alikuwa akielekea katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atatumbuiza leo (Julai 27) na kesho (Julai 28).
Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema Diamond alitakiwa kuondoka jana Saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00 jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.
“Ni kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,” anasema.
Hata hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.
“Ninashauri kama Basata wana chochote wanataka wasanii wakifanye wakishirikishe ili kuepusha mzozo,” anasema