Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:02 pm

BURUDANI: ALICHOKIANDIKA ALIKIBA JUU YA UGOJWA WA OMMYDIMPOZ

Dar es salaam: Mkali wa Bongo fleva nchini Tanzania AliKiba amemfariji kwenye siku yake ya kuzaliwa Rafiki yake wa karibu ambaye wako chini ya Label Moja ya Rock Star Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpozi

Akimtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa leo Sept. 13 Ali ambaye anakipiga kunako club ya Coastal Union ya jijini Tanga amemtaka mkali huyo wa hit maker wa wimbo wa YANJE kumshukuru mungu kulingana na matatizo aliyoyapata kipindi hiki na kusema kuwa mungu ndio muumbaji wa kila kitu.

"Happy Birthday ommydimpoz enjoy your special day bro Na wala Usiwaze.Mwenyezi MUNGU ndie Muumbaji Wa wanyonge Na wajanja . Hivyo basi tunatakiwa tumshukuru kwa kutupa/Na Kutunusuru KWASABABU MUNGU Ana maana yake NA anatupenda Sote ..KAZA" aliandika alikiba kupitia ukurasa wake wa Twitter

Hivi karibu Ommy Dimpoz amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya koo na kufanyiwa operation kadhaa baada ya kudhibitishwa na Daktari wake kuwa alikula sumu kupitia kinywaji.hali iliyowafanya madaktari wao kumtengenezea njia ya pembeni ya kupitishia chakula na kupumulia baada ya ile ya zamani kuonekana inashida

Inasemekana kwa sasa Ommy amesharejea nchini Tanzania akitokea Africa kusini alikokuwa kwa ajili ya matibabu ingawa hajafikia nyumbani kwake kwa siku zote.