- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BUNGE LA SENETA: MWANA MFALME SALMAN ALIAMURU MAUWAJI YA KHASHOGGI
Idadi kubwa ya Maseneta nchini Marekani wanaamini pasi na shaka sasa kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman ndiyo alieamuru mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia Nchini Uturuki.
Msimamo huo wa maseneta unakuja baada ya kufanya kikao cha siri na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Bi Gina Haspel.
Seneta wa mwenye ushawishi mkubwa kutoka chama cha Republican Lindsey Graham amesema ana "imani ya hali ya juu" kuwa Mohammed bin Salman (MBS) alipanga njama ya kumuua Khashoggi.
Seneta huyo wa jimbo la Carolina Kusini amesema bin Salman ni "chizi" na "mtu hatari".
Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.
Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.
Mkurugenzi wa CIA bi Haspel alikutana jana Jumanne na wajumbe wa Seneti wa Kamati ya Mambo ya Nje ambao hawakumung'unya maneno baada ya mkutano huo.
"Hapa hakuna bunduki inayofuka moshi - kuna msumeno unaofuka moshi," amesema Seneta Graham akimaanisha mauaji ya Khashoggi yanayodaiwa kutekelezwa kwa kumny'onga kisha kumkata mwanahabari huyo vipande kwa kutumia msumeno.