Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:30 am

BREAKING: ZITTO AKAMATWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU MAUWAJI YA WATU 100

Dar es salaam: Kiongozi wa Chama, cha ACTWazelendo ambaye Pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mh Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam muda huu kwa maelezo kuwa anakwenda kuhojiwa Juu ya mauaji ya Polisi na Raia 100 yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.

Jana Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma lilimtaka mbunge huyo kudhibitisha mbele ya Jeshi hilo kwa kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 walifariki Dunia.

Kama utakumbuka juzi siku ya Jumapili Oktoba 28,2018, Mbunge huyo alizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.

Lakini kwaupande wa Jeshi hilo Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha tuhuma alizotoa Zitto na kusema hazina ukweli wowote.

Alisema hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

“Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”amesema Ottieno.