- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BOBI WINE: NIWAKATI UMEFIKA KWA VIJANA KUCHUKUA UWONGOZI
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine, anasema wakati umefika kwa vijana kuchukua nafasi za kuongoza mataifa ya bara la Afrika.
Kyagulanyi ambaye pia ni mwanamuziki, amekuwa ziarani nchini Kenya akikutana na kutoa mihadhara kwa vijana baada ya kualikwa na muungano wa wabunge vijana nchini humo
“Muda mwingi wa maisha yangu, nimeishi katika mtaa wa mabanda wa Kamwookya jijini Kampala, nikiwa na mama yangu ambaye alikuwa Muuguzi katika Hospitali ya Mulago,” alisema Wine
Aidha, amebaini kuwa mama yake alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 15 lakini baba yake alifariki dunia miaka mitatu iliyopita.
Kabla ya kuanza harakati za kisiasa amekuwa mwanamuziki akiimba kuhusu masuala mbalimbali hasa mapenzi, lakini alibadilisha uimbaji wake na kuanza kugusia masuala la kijamii na uongozi bora kwa lengo la kuihamamisha jamii kufahamu haki zao.
“Nimeimba nyimbo nyingi sana, siwezi kukumbuka idadi,”
“Licha ya kuzaliwa katika familia ya kawaida na kuishi Ghetto, nilihakikisha kuwa naupiku umasikini kwa sababu nilikuwa mbunifu,” aliongeza kwa msisitizo.
Kuhusu namna muziki, ulimsaidia, Bobi Wine, amemwambia Mwandishi wetu kuwa, umemsaidia sana na kubadilisha pakuwa maisha yake.
'Muziki umenifanyia mambo mengi sana, umaarufu lakini pia kufahamika na watu,” alisema