Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 8:50 am

AFYA: WAWEZA KUKOSA AJIRA KAMA UMEJICHUMBUA AMA UNA MICHIRIZI YA MWILI.

GHANA: Kitengo cha uhamiaji nchini Ghana kimewaondolea vigezo waliotuma maombi ya kazi wakati wa zoezi la kukusanya wafanyikazi wapya kwa sababu ya kubadilisha rangi ya miili yao ama maarufu kujichubua na wenye michirizi mwilini.

Msemaji wa kitengo hicho ameiambia BBC kuwa wamewaondolea vigezo kwa sababu wanaweza kupata majeraha na kutokwa na damu wakati wa mafunzo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption michirizi ya mwili

Baadhi ya Waghana wamepinga hatua hiyo na kuiita ya kibaguzi huku baadhi wakikasirishwa zaidi na waliondolewa vigezo kwa sababu ya kuwa na michirizi mwilini.

Nao baadhi wamesifia hatua ya kuwaondelea vigezo waliobadili rangi zao za mwili.

Walioondolewa vigezo, wengine ni wenye michoro mwilini (tattoo) na wenye rasta.

Wanaotuma maombi ya kutraka ajira wanapitia vipimo vya mwili na afya kama sehemu ya zoezi la kuwachuja wenye vigezo.

Watu 84,000 walituma maombi ya kazi hiyo, huku wanaohitajika wakiwa ni 500 pekee.

Mbunge mmoja, Richard Quashigah, amesema kuwa waombaji waliokataliwa wanaweza kuwapeleka waajiri hao mahakamani.