November 28, 2024, 2:26 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
AFYA: UKWELI KUHUSU KONDOM.
Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu kondom na matumizi yake na umeelewa, hujaelewa, umeamini, hujaamini na kadhalika. Lakini ukweli wote kuhusu kondom ni huu.
- Faida za kondom ni kubwa sana kuliko hasara au mapungufu yake
- Kondom hutengenezwa mahsusi kwa ajili ya kutukinga dhidi ya magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya kujamiiana pamoja na mimba. Magonjwa hayo ni kama vile kisonono, kaswende, homa ya ini, ukimwi na kadhalika. Kwenye upande wa mimba kondom husaidia kuzuia mbegu za kiume kufikia mbegu za kike, hivyo kuzuia mimba kutungwa
- Kondom husaidia kupunguza uwezekano wa kupata hayo magonjwa na mimba. Ufanisi wake sio 100%, na huzidi kupungua zisipotumika vizuri
- Ufanisi wa kondom hutegemea na jinsi itakavyotumika. Ikitumika vizuri husaidia sana na ufanisi wake huwa mkubwa sana. Husaidia kuzuia virusi vya ukimwi, kisonono, kaswende, homa ya ini na magonjwa mengine. Pia husaidia kuzuia mimba. Ikitumika vibaya haiwezi kusaidia vizuri kuzuia magonjwa na mimba
- Watu wengi hupata mimba na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana kwa sababu hawatumii kabisa kondom. Wachache hupata kwa sababu hawatumii vizuri
- Kabla ya kuruhusiwa kuingizwa nchini na kutumiwa na wananchi kondom hufanyiwa ukaguzi na vipimo vya ubora na usalama na mamlaka za serikali. Hii husaidia kudhibiti kondom zisizo na ubora na zile zisizo na usalama.
- Kondom zote zilizokaguliwa na kuruhusiwa kutumika na wananchi ni bora na salama. Usiwasikilize wala kuwaamini watu wanaodanganya kuwa kondom zina virusi vya ukimwi au matobo yanayopitisha virusi vya ukimwi
- Kuna watu wenye imani potofu au ukosefu wa elimu na wanapotosha kuhusu kondom. Watu hao waelimishwe au wasisikilizwe au wapuuzwe
- Kondom huweza kuchanika au kuharibika zikitumika vibaya. Hapo kinga yake hupungua na mimba huweza kutungwa au maambukizi kuweza kutokea
- Kuvaa kondom zaidi ya moja haiongezi ufanisi wa kinga dhidi ya mimba au magonjwa, ndo kwanza hupunguza
- Â Tofauti ya bei za kondom aina mbalimbali inachanganya sana watu wengi. Je, zenye bei kubwa ndio bora na salama kuliko zenye bei ndogo? Zenye bei ndogo au zinazogawiwa bure ni bora na salama kwa kiasi gani?
- Tofauti ya bei za kondom hutokana na sifa za ziada zinazoongezewa, hususan kuongeza msuguano na ladha wakati wa kufanya mapenzi. Hii ndio sababu kwa nini kondom nyingi zenye vinundu vinundu (vipele) huwa na bei kubwa kuliko zile za kawaida zisizo na vipele au vinundu nundu
- Kuna kondom za kike na za kiume. Akivaa mwanamke basi mwanaume asivae, na akivaa mwanaume basi mwanamke asivae
- Kila kondom moja ni kwa ajili ya tendo moja tu. Usitumie tena kondom mara baada ya kuitumia awali. Kondom isifuliwe na kuanikwa kwa ajili ya kutumiwa tena
- Kondom huweza kuchanwa kwa kucha. Hakikisha vidole havina kucha ndefu au kucha hazishiki kondom yako
- Baadhi ya watu hawapendi kondom. Hawa wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya zinaa na mimba zisizopangiliwa
- Kondom hupunguza kidogo msuguano kati ya uke na uume. Hii hupelekea wengi kuhisi ladha ya tendo la kujamiiana kupungua
- Kondom haipunguzi sana ladha ya mapenzi kama wengi wanavyohisi au kusema. Kwa kiasi kikubwa hilo huchangiwa na saikolojia ya mtu. Ukiambiwa kondom hupunguza ladha nawe ukaamini hivyo basi ukija kutumia utaona kweli
- Kondom ni njia nzuri sana kwa ajili ya kupanga uzazi. Inaweza ikatumia muda wowote na siku yoyote. Ikitumika vizuri uwezekano wa kupata mimba ni mdogo sana, karibu na hakuna
- Kondom zina tarehe ya mwisho wa matumizi pia. Usitumie kondom ambayo muda wake wa matumizi umeisha
- Kondom huweza kutumika vibaya na watoto, kuchukiwa na watu wengine na hata kuziba vyoo. Hifadhi kondom zote vizuri mbali na watoto na watu wengine, pia itupe vizuri ili isizibe choo
Huo ndo ukweli kuhusu kondom. Inawezekana kukawa na zaidi ya hapo, nasi tunakaribisha mjadala, maswali na maoni zaidi. Karibu sana.