- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
AFYA: NJIA ASILI 12 ZA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI.
Kuna mtu alinitumia ujumbe mfupi juzi kati hapa kwamba, dokta wake kamwambia aache kutafuna chewing gum na kufyonza pipi hizi,ambayo ilikua ikimsababishia tumbo kujaa gesi.(Nikaiangalia hiyo nikaona na kutokana na Mayo Clinic,yote ni sawa na ni kisababishi kikubwa kwa watu wengi tu kwasababu unavuta hewa…kufyonza mrija pia ni sababu ya gesi).Anyway,aliniuliza kama najua tiba yoyote ya asili ambayo inaweza kuwa kitunguu au kituungu thoum ili aondoe harufu ya mdomo, tokea apo hivyo ndio viungo anavyovipenda yeye.(mimi mwenyewe nimeanza kutumia hizi).
Kwahiyo nikafanya uchunguzi ,kujaribisha mawazo mengi mengi tofauti,nikaona nisiwe mchoyo nanyi muyajue.Nahisi tumbo langu limeshachoka na hizi kahawa nazokunywa!Labda utafiti mwingine ujao utaangalia jinsi ya kutoa caffeine baada ya kuwa nyingi tumboni,sijajua athari kuhusu kama vitunguu,tangawizi ,viungo,n.k.
CHAI YA KIJANI(GREEN TEA) - Green tea ni tajiri wa polyphenol,ina antioxidant yenye nguvu sana ambayo itaondoa plaque kuenea kwenye meno yako. Polyphenols imeonekana kuzuia bacteria kukua katika mdomo.Kwahiyo kufyonza chai ya kijani husaidia kuondoa harufu chafu ya vitunguu.Spinach ,chai ya rangi,apples na mushrooms pia nazo zina polyphenols, unaweza pia kutumia aina hii ya vyakula na kinywaji baada ya kujiona mdomo unatoa harufu iliosababishwa na mlo wako.Mimi binafsi napenda chai labda inanisaidia.
MATUNDA NA MBOGA FRESH – Fiber-nyingi hupatikana kwenye matunda na mboga, husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomoni(na kujisikia umeshiba muda wote,ambayo husaidia kupunguza uzito).Fiber kwenye vyakula vingi husaidia kutengeneza mate,ambayo husaidia kusafisha plaque zinazojijenga.Fiber imo kwenye vyakula kama cerely,apples,na karoti.Enzymes wa asili wanaptikana kwenye apples ,berries,nanasi,na kiwi huondoa sulfur compounds na huondoa harufu mbaya ya mdomoni.Mboga zenye vitamin C,kama red bell peppers na broccoli husaidia kutengeneza mazingira ya kuzuia bacteria wa mdomoni,pindi inapoliwa hufanya kazi hiyo.Hivi vyakula pia husaidia kuondoa mabaki ya vyakula katika meno pia.
MKATE –Kukosa carbs katika mlo wako huchangia harufu mbaya ya mdomo.Kula kipande cha mkate husiadia kuleta harufu nzuri mdomoni.Baada ya kula kipande cha kitunguu,kipande cha mkate kitasaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni,lakini ladha hubakia kwenye ulimi.Hata hivyo ukila kipande cha mkate huondoa hiyo harufu na utakua umehifadhi calories kwa matumizi mengine.
MITI SHAMBA FRESH – Kabla ya mouthwash hazijajulikana,watu walikuwa wakitafuna miti shamba kuondoa harufu mbaya.Miti shamba ina chlorophyll,ambayo huondoa harufu na uchafu.Aina ya mitishamba mizuri na fresh ni mkama parsley,mint,binzari,basil,rosemary,thyme,tarragon na cilantro.Kama chakula chako kitakua na aina yoyote ya miti shamba tafuna kwa kuondoa harufu.Baada ya chakula pia unaweza tafuna yoyoteambayo unao uwezo wa kuipata na huondoa harufu mbaya mdomoni.
HARADALI(MUSTARD) – Ok,hii ni ngumu kujaribu lakini pia ijaribishe.Kuna njia mbili tofauti zipo katika haradali( mustard).Kwanza,chukua kijiko cha chai cha haradali weka mdomoni,sukutua kisha tema kwa dakika chache.Kisha chukua nusu kijiko cha chai cha haradali meza itaenda tumboni ambapo itaenda kuua harufu ya vitunguu thoum na vitunguu mwilini.Njia ya pili ,kuchanganya vijiko vya chai viwili vya mafuta ya haradali na chumvi.Kisha weka mdomoni huku ukichezea ndani ya mdomo,tema mate yatayojitokeza na iache haradali kwa dakika 30 .
MAZIWA YA MTINDI –Ounches sita za maziwa ya mtindi husaidia kuondoa harufu mbaya na uchafu ambayo husababisha hydrogen sulfide na huua wadudu wa mdomoni. Tumia kwa kunywa maziwa ya mtindi kila siku.
MBEGU & KAHAWA(COFFEE BEANS) –Kutafuna karafuu,au hiliki,shamari(fennel),mbegu za anise, mara moja huondoa harufu mbaya mdomoni.Kama unahisi unatatizo la aina ya vyakula kwa sababu ya meno,kuwa makini na hizi pia.Kula kahawa(coffee beans) ilo kaushwa ni nzuri zaidi na huondoa harufu kwa haraka zaidi.
NDIMU – Kulamba ndimu au kutafuna ganda dogo la ndimu ni nzuri kwa kuondoa harufu mdomoni pia.Lakini juisi ya ndimu ina acid na huweza kuwa mbaya kwa meno yako,husababisha meno kupata ganzi.
JUISI YA SIKI YA APPLE – Ni nzuri!Sio tu kwa ajili ya kusukutua ½ kijiko cha chai cha juisi ya siki ya apple iliochanganywa na kikombe cha maji,husaidia harufu pia,huondoa harufu ya vitunguu na huwa ni ladha pia ulimini.Kuchanganya na maji,huondoa ule ukali wake na utausikia mdomo uko vizuri mwepesi.Naifanyia kazi post zijazo kuhusu juisi ya siki ya apple na matumizi yake.
BAKING SODA – Kutengeneza mouthwash ya baking soda na maji ni tiba ya asili ya muda mrefu.Tumia hii kwa kusukutua mara moja kwa siku.
Of course kupiga mswaki meno yako,mouthwash,flossing na kusafisha ulimi utaweka mdomo wako kuwa na harufu nzuri na fresh na pia huwa oral hygiene mzuri.
Harufu mbaya ya mdomo inakera ukiangalia vyakula vyenyewe hivi vya viungo na uzembe wa usafi unaoweza sababisha hata ukavu wa mdomo,vijidudu vya kwenye fizi, na vijidudu.Kama utagundua tatizo hili la harufu mdodmoni inaendelea,muone daktari wa meno kwa tiba na ushauri zaidi.