- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
AFYA: MAUMIVU YA TUMBO KIPINDI CHA HEDHI.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Takribani nusu ya wanawake wote waliopo katika umri wa kuweza kupata mototo wanakumbana na maumvu wakati wa hedhi, maumivu ambayo huanza siku chache kabla ya hedhi na kuendelea kwa siku kadhaa. Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kawaida lakini kwa wengine maumivu huwa makali sana hadi kupelekea kushindwa kufanya shuguli zao. Hii ni moja ya sababu watoto wa shule kukosa vpindi kwa siku kadhaa. Ili kupata tiba basi wanawake wengi hukimbilia kunywa dawa za kupunguza maumivu na baadhi ya madactari hutoa ushauri wa kunywa vidonge ili kuzuia hedhi ili kupunguza makali ya maumivu, njia zote hizi mbili zikiwa na madhara na pia kutoweza kutoa suluhisho ala kudumu la tatizo husika.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
• Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.
• Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.
• Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).
• Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Maumivu ya Tumbo la Hedhi... Sehemu ya Pili
Hii inahusisha magonjwa ambayo husababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
• Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.
• Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.
• PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga
• Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
• Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.
Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo,
hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?
1. Maumivu mara nyingi si makali.
2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti
3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.
4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.
5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.
7. Kufunga choo.
8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.
9. Kuhisi maumivu ya kichwa.
10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.
Inapasa kujua kuwa, kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hutambua wanapopata tumbo la hedhi bila hata msaada wa daktari. Wanawake wanashauri iwapo watapata maumivu makali sana ni bora wakamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo matatizo mengine ya kitiba yanayosababisha maumivu hayo kuwa makali.
Kuna baadhi ya tiba za mitishamba pia ambazo husadia kupunguza muamivu ya tumbo la hedhi. Hapa namaanisha herbal, wenzetu Wachina ni watalamu wazuri katika ujuzi huo unaweza kuagiza kutoka ofsini kwetu moja kwa moja na ukazipata. Vilevile wanawake washauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu hayo, baadhi ya hivyo vimetaja kama kuoga maji moto, kutumia hot bottle na hata kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo. Kuna baadhi husaidia kwa kufanya mazoezi kama yoga, meditation, kusuliwa, tiba ya sindano (Acupunture), au kushituliwa mishipa ya fahamu ( Transcitaneous Electric Nerve Stimulation na hata wengine husaidiwa kwa tendo la kujamiiana. Vilevile kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.
Tunaelezwa kuwa tunaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kuacha kunywa vinywaji ambavyo ni high fructose corn syrup( juis na soda zote) pombe, cofeini, Sodium na sukari.
Kufanya mazoezi.
Kujiepusha na wasiwasi na mawazo.
Kuepuka kufuta sigara.
VITAMINI D
Sasa watafiti wamegundua njia ingine ambayo ni salama kwa ajili ya kupunguza maumivu makali wakati wa hedhi ambayo ni Vitamin D kutoka kwenye jua. Wakati wa hedhi mfuko wa mimba hujipunguza kwa kumomonyoka endapo yai halikurutubishwa, kumomonyoka huku huletekezwa na kichocheo kinachoitwa prostaglandin. Hvo kiasi kikubwa cha kichocheo hiki basi hupelekea ,maumivu kuwa makubwa zaidi. Vitamin D itakusaidia kupunguza uzalishaji wa homoni hii ya prostaglandin. Watu wengi wana upungufu wa vitamin D kutokana na kutotumia mda mwingi kupata mwanga wa jua na hivo kupelekea pia matatizo mengine ya kiafya kama magonjwa ya shinikizo la damu na saratani pia. Hivo hakikisha kila siku unatumia mda wa kutosha kupata mwanga wa jua la asubuhi ama jioni
kwa wale akina mama wenye matatizo ya homoni, kuvurugika kwa hedhi na kukosa ujauzito kwa mda mrefu basi tumewaandalia programme ya week 3 ambayo itakusaidia kubalansi homoni zako na kurejesha uwezo wa kushika ujauzito. Tunashauri wanandoa wote kufanya vipimo ili kujua chanzo cha tatizo lako la kushindwa kushika ujauzito. karibu nawe upate huduma hii ya virutubisho na dawa zetu za asili ili uwe mmoja wa mashuhuda na mwenye furaha kama baadhi ya hawa wagonjwa tuliokwisha kuwapa huduma.