- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
AFYA: MADHARA YA KUKOSA CHOO KWA MUDA MREFU
Mwili wako ni mfano wa silinda kubwa ambayo ndani yake kuna tube inayoanzia mdomoni mpaka chinikwenye puru pale unakotolea uchafu, silinda hii ndio mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hivyo mfumo wa chakula upo ndani ya mwili na umesheheni kemikali mbalimbali ambazo husaidia usagaji na uchkataji wa chakula ili kupata virutubisho vinavyohitajika na mwili. Mfumo wa chakula unachangia karibu asilimia 80 ya utimamu wa afya yako . usagajiwa chakula huanzia mdomoni pale unapotafuna chakula na kikachanganyika na mate.
Usagaji na uchakataji wa chakula huishia kwenye utumbo mpana baada ya mwili kufyonza virutubisho muhimu na maji na kuacha takataka ambazo hazitumiki, virutubusho ambavyo vinavyonzwa ili kutoa energy ambazo ndio tunaita kalori. Kalori kiasi gani unakula na pia ubora na chanzo cha kalori ama chakula unachokula ni sababu za msingi ambazo zinaathiri afya yako aidha chanya au hasi. Sababu nyingine ambayo inaleta matokeo kwenye afya yako na hatari ya kupata cho kigumu ni kiasi na aina ya bacteria waliopo katika mfumo wako wa chakula. Bacteria hawa wamegawanyika sehemu mbili kuna bacteria wazuri ambao husaidia usagaji wa chakula na bakteria wabaya ambayo ndio chanzo cha matatizo ya tumbo na utumbo, kusababisha aleji, uzito mkubwa na kitambi pamoja na matatizo mengine mengi. Watafiti waligundua kwamba pale ambapo msongo wa mawazo huleta athari katika mfumo wa chakula basi ndivyo pia mfumo wako wa chakula unavoweza kuleta athari katika ubongo ikiwemo kumfanya mtu kuwa na hasira, kwa maneno mengine tunaweza kusema hivi mfumo wako wa umeng ‘enyaji chakula siyo tu unahishwa na matatizo kama kukosa choo/choo kigumu, kuharisha, uzito mkubwa na kitambi ni zaidi ya hapo hata maamuzi yako yantegemea pia vyakula unavyokula.
MAKUNDI YA WATU WALIOPO KATIKA HATARI YA KUPATA CONSTIPATION NA KWANINI??
Baadhi ya visababishi vya kukosa choo ama kupata choo kigumu ni kama matumiz ya muda mrefu ya vidonge mfano vidonge vya kupunguza tindikali tumboni, ufanyaji kazi mdogo wa tezi ya thairodi (hypothyroidism), magonjwa ya mfumo wa chakula kama irritable bowel syndrome(IBS), kuchelewa kutoa haja mfano mtu anapojizuia kutumia vyoo vya umma. Cha kukumbuka ni kwamba moja ya chanzo cha haya yote ni lishe, sanasana kama lishe yako inategemea zaidi vyakula vilivyosindikwa na vyenye nyuzinyuzi kidogo. Yafuatayo ni magroup ya watu waliopo katika hatari zaidi ya kupata constipation
- 1.WANAWAKE, zaidi wanawake wenye ujauzito na baada tu ya kujifungua. Uzito wa mtoto hukandamiza utumbo na hivo kupunguza usafirishaji wa choo kwenye utumbo na hivo kupelekea maji mengi kufyonzwa. Nb napenda msomaji ufahamu kuwa maji hufyonwa kwenye utumbo mpana ambako choo kinakaribia kutoka, hivo choo kinavokaa zaidi bila kutolewa ndivo maji yake hufyonwa zaidi na kukifanya kiwe kigumu kama cha mbuzi.
- 2. WAZEE wapo katika hatari zaidi ya kupata constipation kwa sabau ya kupungua kwa kasi ya kazi za mwili na hvo kupunguza kasi ya usafirishaji katika mfumo wa chakula.
- 3.WATU WENYE KIPATO KIDOGO kutokana na kutokuwa na uwezo wa kununua vyakula salama na asili visivyosindikwa
- 4.Waliofanyiwa upasuajikutokana na kwamba hawafanyi kazi mda mwingi wametulia na hivo kupelekea kasi ya usafirishaji wa choo pia kupungua.
UHUSIANO KATI YA CONSTIPATION NA AFYA YA MWILI
Kupata choo kigumu ambako kunapelekea mtu kutumia nguvu nyingi kujikamua ili kutoa kinyesi kunaweza kukusababishia kupata ugonjwa wa bawasiri ama Hemorrhoids ambapo ni matokeo ya kutanuka kwa mishipa ya damu, kutanuka kwa mishipa hii ya damu hupelekea kinyama kuota aidha ndani au nje ya sehemu ya haja kubwa na kupelekea maumivu makali. Pia constipation ya mda mrefu inaweza kupelekea Via vya uzazi kwa mwanamke, hii ni kutokana na kwamba sehemu ya uzazi na ile ya haja kubwa zipo karibu sana, presha inayotengenezwa baada ya kusukuma choo kwa nguvu basi inaweza kupelekea kulegea kwa mishipa na kuweza kuleta matatizo kama kurudi kwa mkojo kwenye figo ambayo inaweza kuleta matatizo ya moja kwa moja ya figo. Hivo unapopata haja basi usikawie kutoa maana kukaa mda mrefu kutasababisha uchafu mwingi kukusanyika na hivo ukatumia nguvu nyin haja gi kusukuma uchafu, ambapo wakati mwingine hii inaweza kuleta shida na utumbo ukatoka nje ya njia ya haja kubwa.
MTINDO WA MAISHA UTAKAOKUSAIDIA KUTIBU TATIZO
Kwa ambaye tatizo limekufikia hatua mbaya basi suluhisho lako ni kubadili mfumo wa maisha ikiwemo kwenye lishe, hatua ya kwanza na rahisi ni kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha bonyeza link hyo kufahamu faida na kiasi cha maji unachotakiwa kunywa pili matumizi ya vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi husaidia katika kuleta shape ya choo na kuepuka choo kigumu,hakikisha kila siku unakula vyakula gramu 30 mpaka 32 vyenye nyuzi nyuzi mfano mboga za majani.
mazoezi ya mwili husaidia kurahisisha usafiri na utoaji wa takamwili kiurahisi hivo weka ratiba walau mara 3 kwa week kufanya mazoezi na Nne vyoo vya kukalia ni hatari kwa afya yako kwani vinakusababishia matumizi makubwa ya nguvu wakati wa kujisaidia na hivo kupelekea constipation na matatizo mengine kama bawasiri, tumia vyoo vya kawaida vya kuchuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa. Kama tatizo ni kubwa basi unaweza kutujulisha ukafika ofsini kwetu na ukajipatia dawa za mimea.