November 26, 2024, 9:17 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ZITTO KABWE "TUMEKABIDHI NCHI KWA WASHAMBA NA MALIMBUKENI WA MADARAKA"
Dodoma: Mbunge wa Kigoma Ujiji Zitto Zuberi Kabwe ameongea maneno magumu juu ya tawala za mihimili mitatu ya nchini, Zitto amesema kuwa kwa awamu hii nchi imekabidhiwa kwa watu anao waona kuwa ni jamii ya wasiojui mambo(washamba) na ambao ni malimbukeni wa madaraka "Tumekabidhi nchi Kwa washamba na malimbukeni wa madaraka. Mihimili karibu yote ya dola letu inaongozwa na malimbukeni".
Akitumia ukurasa wake wa facebook Zitto amesema kuwa waerevu wengi nchini wananyamanzishwa na viongozi walio juu ya madaraka, waerevu hao wanaitwa wao sio wazalendo wa nchi hii."Tumekabidhi nchi Kwa washamba na malimbukeni wa madaraka. Mihimili karibu yote ya dola letu inaongozwa na malimbukeni. ' wajanja ' wanalamba miguu ya washamba ili kuishi tu. Werevu wananyamazishwa, wanaitwa si Wazalendo. Wanapangiwa mauaji. Nchi imewashinda".
Zitto anaona kuwa nchi inabidi ijiandae na anguko la kiuchumi kwa sababu ya kukosa maamuzi sahihi ya kimaendeleo "Anguko kubwa la uchumi laja sababu ya maamuzi ya kishamba na kukosa maarifa. Hata hivyo watabaki werevu kadhaa na watarejesha nchi yetu kwenye mstari". alimalizia Zitto
Zitto anatuhumiwa na spika baada ya kumkosoa kupitia mitandao ya kijamii, kuwa bunge limewekwa mfukoni na muhimili mwingine wa nchi. Zitto anatarajiwa kuungana na Mbunge mwenzake wa Upinzani ambae ni mbunge wa Ubungo Said Kubenea katika kamati ya maadili hii. Kubenea alifikishwa jana kwenye kati ya maadili kutokea Dar es salaam lakini walishindwa kumuhoji kwa sababu ya kujisikia vibaya kiafya.