Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 9:23 am

NEWS: TSHISEKEDI ACHAGULIWA TENA KUGOMBEA URAIS NCHINI CONGO

DRC Congo. Wajumbe wa mungano wa chama cha kisiasa cha Union Sacree unaohusisha wanasiasa wa Kongwe na maarufu nchini Congo kama waziri wa ulinzi Jean Pierre Bemba na waziri wa uchumi Vital Kamerhe, wamemchagua Rais wa sasa wa Congo Felix Tshisekedi kwa sauti mmoja kuwa Mgombea wao wa Urais wa nchi hiyo.

DR Congo: Tshisekedi takes office, but Kabila's legacy casts long shadow

Tshisekedi anagombania mhula wa pili katika taifa lenye utajiri mkuu wa cobalt duniani, baada ya kushinda katika mhula wa kwanza ulokuwa na utata mwaka 2018.

Utawala wake umekumbwa na hali ngumu ya uchumi, janga la Covid 19, mlipuko wa Ebola, ukosefu wa usalama hasa mashariki ya nchi ambako wapiganaji wa kundi la M23 waliteka sehemu ya maeneo ya mashariki na kusababisha kuvunjika kwa uhusiano na Rwanda.

Tshisekedi, kijana wa mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Etienne Tsisekedi, aliyeahidi kupambana na ulaji ushwa na utawala wa kimabavu anakanusha tuhuma kutoka makundi ya kutetea haki za binadama na wakosowaji wake, kwamba ameshindwa kutekeleza ahadi zake.

Tshisekedi anagombania mhula wa pili katika taifa lenye utajiri mkuu wa cobalt duniani, baada ya kushinda katika mhula wa kwanza ulokuwa na utata mwaka 2018.