Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:45 pm

ZITTO KABWE: "HATUJAWAHI KUWA NA SPIKA ANAYEDHALILISHWA NA RAIS"

Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma Ujiji Kupitia tiketi ya chama cha ACT wazalendo Mh. Zitto Zuberi kabwe ameonesha kukasirishwa na spika wa bunge Job Ndugai kwa madai yakuwa bunge halijitegemea kama muhimili na badala yake linapangiwa mambo na Rais wa Jamhuri "Hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa Na Rais Kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge"


akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Zitto amesema kuwa kwahali ilivyo hivi sasa spika ndugai hajafikia hata asilimia 10% ya uwendeshaji kibunge kama ilivyokuwa kwa Samweli Sitta na Anna Makinda mpaka sasa "Kwenye mazishi ya Spika wa Watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 Sasa"


"Spika Ndugai angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya, Wabunge wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na Spika Ndugai tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu. Anatuangusha" ameongea Zitto


Zitto amesama kuwa Spika Ndugai ndie spika wa kwanza katika historia ya Tanzania mbuge wake kushambuliwa na Risasa na watu wasio julikana "Spika Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya Nchi yetu kushuhudia Mbunge anapigwa risasi Mkutano wa Bunge ukiendelea"

kama utakumbuka sakata analolizungumzia Zitto ni Lile la mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu kushambuliwa na Risasa mnamo Tarehe 7 mwezi 9 mwaka huu nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Imeandikwa na Deyssa h. deyssa

muakilishi publisher