Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:56 pm

YAFAHAMU MAMBO 11 WALIYO KUBALIANA RAIS MAGUFULI NA RAIS ZUMA

Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jana alifanya mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Afrika kusini Bw. Jakob Zuma, ambapo wamekubaliana kushirikiana katika maeneo makuu 11 yakiwamo ya biashara, uwekezaji, afya, elimu, sayansi, teknolojia, uchumi wa viwanda, ulinzi na usalama, utalii na madi.

Rais Magufuli akiambiwa jambo na Mgeni wake Rais Zuma

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mapendekezo yaliyo amualiwa na mawaziri wa nchi hizo mbili wa Mambo ya Nje na kuridhiwa rasmi jana katika mazungumzo ya ndani ya Rais John Magufuli na Rais Jacob Zuma, Rais ZUMA alikuwa na ziara ya kikazi nchini ya siku mbili kuanzia juzi.

Rais Zuma akisalimia viongozi wa Tanzania

Aidha, katika kikao hicho cha ndani, Dk Magufuli alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Zuma ambaye pia ni mwanachama wa jumuiya ya nchi tano zenye nguvu kiuchumi duniani (BRICS), Aiombee mkopo wenye Riba nafuu kwaTanzania kwa ajili ya kumalizia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge.

Maraisi wa nchi za BRICS

Naye Rais Magufuli akiongea na waandishi wa Habari Ikulu aliyaelezea mapendekezo hayo ya mawaziri kuwa yatasaidia nchi hizo hasa Tanzania katika kukuza uchumi wake. Rais Magufuli alisema mawaziri hao walipendekeza nchi hizo ziendelee kushirikiana katika eneo la biashara na uwekezaji ambapo kwa mwaka jana pekee, biashara baina ya nchi hizo ilifikia thamani ya Sh tilioni 2.4 huku uwekezaji wa Afrika Kusini nchini Tanzania ukifikia Dola za Marekani milioni 800.15 na kutengeneza ajira 20,616.

“Tumekubaliana pia katika eneo hili nchi zetu ziondoe vikwazo vyote ambavyo vinakwamisha biashara kati yetu,” alieleza Magufuli. Alisema katika eneo la uchumi wa viwanda, nchi hizo zimekubaliana kupitia mkakati wa Maendeleo ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)