- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI KALEMANI: TANZANIA INAONGOZA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AFRIKA
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani, amesema Tanzania kwasasa inashika namba moja Afrika katika kusambaza umeme vijijini ikiwa imefikia asilimia 74 ya vijiji vyote nchini ikifatiwa na Nigeria yenye asilimia 72.
Waziri Kalemani alisema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
“Awali, Nigeria ndiyo ilikuwa ikiongoza ikiwa na asilimia 72 lakini tumeipita, tukiwa tumefikia zaidi ya asilimia 74 na hivyo tunaongoza Afrika kwa sasa,” amesema Waziri.
Dk Kalemani alisema vijiji 9,001 nchini vimeshaunganishiwa umeme na kwamba na kati ya hivyo, 3,559 vimeunganishiwa umeme kupitia Mzunguko wa kwanza wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa Umeme Vijijini (REA III-1), unaoendelea hivi sasa.
Alisema mradi wa REA III-1 utakamilika Juni lakini Serikali imekubaliana na wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo nchi nzima, kukamilisha kazi husika miezi miwili kabla, hivyo wanatarajiwa kukabidhi kazi kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ifikapo Aprili 31.
Kwa upande wa Wilaya ya Masasi, Dk Kalemani alisema Serikali iliamua kurejea mpango-kazi na kufanya mabadiliko ambayo yaliwezesha kuongeza idadi ya vijiji vitakavyonufaika na mradi huo wilayani humo.
“Katika mpango wa awali ni vijiji vichache tu vya Masasi ndivyo vilikuwa vinufaike na mradi huu. Hii ni kwa sababu vijiji vingine viko katika halmashauri za miji na siyo wilaya hivyo vilikuwa vinakosa sifa kwani vilikuwa na hadhi ya mitaa na siyo vijiji.”
Akijibu hoja za wananchi wa vijiji vya Namikunda A na B, Nagaga na Matogolo kuhusu changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara, alisema tayari Serikali imeshughulikia tatizo hilo kwa kuunganisha baadhi ya maeneo ya Mtwara katika gridi ya taifa.
Aliyataja maene hayo kuwa ni Tunduru, Masasi na Nanyumbu na kwamba yameunganishwa kupitia mradi wa umeme mkubwa wa Makambako – Songea (kilovoti 220