- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI KALEMANI: NENDENI MKAWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU WOTE
WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani, ameliagiza Shirika la Umeme nchini ( TANESCO) kuendelea kukata umeme mara moja kwa wadaiwa sugu wote ili kuweza kukusanya mapato zaidi na kulipa madeni ya shirika hilo.
Dk. Kalemani alisema hayo, jijini Dodoma alipokutana na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO, kuzungumzia tathimini ya miaka mitano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kiuo cha kupoza na kuzambaza umeme cha Zuzu.
Dk. Kalemani aliiagiza TANESCO kulipa madeni inayodaiwa na kutoongeza madeni mapya, vilevile wadaiwa sugu wakumbushwe madeni yao na endapo hatawalipa, wakatiwe umeme.
“TANESCO inadaiwa madeni makubwa pia yenyewe ina wateja wengi sana ambao ni wadaiwa sugu wanaodaiwa fedha nyingi na hawalipi, zimo taasisi, mashirika ya umma na binafsi na watumiaji wa kawaida, ninawaagiza nendeni mkawakatie umeme. Narudia tena mkakate umeme, mkishaukata, wahusika watalipa na wataonyesha ushirikiano tofauti na kumdai kawaida tu”, alisema Dk. Kalemani