Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:29 pm

WATAKAOBAINAKA KUHUJUMU KUKAMATWA KWA NDEGE SAUZI KUSHTAKIWA

Dodoma. Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ameahidi kuwa wale wote watakaobainika kuihujumu Serikali kuhusu kuzuiwa kwa ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) nchini Afrika Kusini watafunguliwa kesi.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan

Abbas amesema watafunguliwa mashtaka ya kuihujumu nchi mara baada ya kumalizika kwa kesi ya kuziwa kwa ndege hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu ya Afrika Kusini.

Kauli ya Dtk Abbas ameitoa leo Jumamosi Agosti 31, 2019 mjini Dodoma huku akisema kuwa wapo Watanzania wanaishiriki kuihujumu Serikali kuhusu ndege hiyo, kwamba kuna siku uhujumu huo utawasaidia.

“Wapo wazawa wanaofanya mawili matatu kuhujumu nchi lakini niwaeleze tusubiri kesi iishe huko Afrika Kusini, tutawafungulia kesi ya kuhujumu nchi yetu.”

“Hakuna Nabii katika historia ya Manabii aliyewahi kuaminiwa kwa asilimia 100, hivyo huwezi kukubaliwa na watu wote, hata hii ndege inayoshikiliwa ikija Tanzania ipo siku wanaochukia watatumia usafiri huo kwenda Afrika Kusini kama sio wao basi watoto wao,” amesema Dk Abbas.

Jana Agosti 30, 2019 Mawakili wanaoiwakilisha Tanzania katika kesi ya kuzuiwa ndege hiyo waliitaka mahakama Kuu ya Afrika Kusini kutupilia mbali zuio la kuzuia ndege ya shirika hilo ya Airbus A220-300, wakisema ilitolewa kimakosa.