Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:01 pm

WANAJESHI WA MAREKANI WALIOATHIRIKA NA SHAMBULIO LA IRAN WAFIKIA 109

Taarifa kutoka Marekani ni kwamba Idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaouguza majeraha ya ubongo kufuatia makombora ya Iran yaliorushwa dhidi ya wanajeshi wa Marekani katika kambi moja nchini Iraq mwezi Januari wamefikia 109, kulingana na taarifa ya maafisa wa Marekani.

Iran iliishambulia kambi hiyo ya wanajeshi wa marekani ili kulipiza kisasi mauaji ya jenerali Qasem Suleimani

Idadi hiyo iliongezeka kutoka wanajeshi 64 walioripotiwa hapo awali na Pentagon.

Kama utakumbuka Rais wa nchi hiyo Donald Trump awali alisema kwamba hakuna raia wa Marekani waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo, taarifa ambayo inaonekana ilikuwa ya uongo baada ya Pentagon kudhibitisha kuwa waathirika ni zaidi ya mia.

Shambulio hilo la tarehe 8 mwezi Januari linajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mauaji ya jenerali mmoja wa Iran. karibia asilimia 70 ya wanajeshi waliojeruhiwa wamerudi kazini , pentagon iliongezea katika taarifa.

Image result for number of america army affected by iran

Mwezi uliopita Rais Trump alipuuzilia mbali uwepo wa majerha ya ubongo alipoulizwa juu ya athari ya shambulio hilo.

"Nilisikia kuwa walikuwa na maumivu ya kichwa, na mambo kadhaa, lakini ningesema, na naweza kuripoti, sio mbaya sana," alisema.

Alipoulizwa kuhusu majerha ya ubongo au TBI alisema: "Sidhani kama ni majeraha makubwa sana ikilinganishwa na majeraha mengine ambayo nimeona."