Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:43 am

WAITARA: MARUFUKU SHULE BINAFSI KUFUKUZA MWANAFUNZI KWA ADA

Dar es Salaam: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amepiga marufuku wanafunzi wa shule binafsi ambao hawajamaliza ada kusimamishwa au kufukuzwa shule.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Januari 10, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waitara amesema kuanzia kesho Ijumaa ataanza kupokea taarifa kutoka kwa katibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri na wadhibiti ubora wa shule ambazo zimewafukuza au kuwarudisha wanafunzi. Amesema ni marufuku mwanafunzi kusimamishwa au kufukuzwa shule kwa sababu ya kutolipa ada bila kujali anasoma shule ya umma au binafsi.

Waitara amesema jambo jingine ambalo Serikali haikubaliani nalo ni la wazazi kulazimishwa kulipa ada kwa mkupuo na iwapo hawajafanya hivyo wanafunzi hawataendelea na masomo hata kama mwaka uliopita walifanya hivyo.

"Nina sms (ujumbe mfupi wa maandishi) nilizotumiwa na wazazi wa shule ambazo zimerudisha wanafunzi nyumbani kwa kukosa ada na malipo mengine ya kiholela kama vile kulazimishwa kununua sare za shule shuleni, for figer, rim na madaftari ya ganda gumu (counter book),” amesema Waitara. “Nataka maofisa elimu, wakurugenzi na makatibu tarafa kwenda kwenye hizi shule (anazitaja shule) hadi kufikia kesho niwe na majibu yanayoonyesha kupatikana ufumbuzi."

“Nataka maofisa elimu, wakurugenzi na makatibu tarafa kwenda kwenye hizi shule (anazitaja shule) hadi kufikia kesho niwe na majibu yanayoonyesha kupatikana ufumbuzi." Waitara pia amewataka wazazi ambao watoto wao wamerudishwa kwa ajili ya kutolipa au kukamilisha ada wafike kwenye ofisi alizozitaja au Tamisemi kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Naibu waziri huyo amesema kuna haja ya kurudisha mjadala wa ada elekezi.

"Nafanya utaratibu kurudisha mjadala wa kuangalia namna ambavyo Serikali itatoa msimamo wa ada elekezi kwa sababu kuna shule zinatoza kuanzia Sh1.5 milioni hadi Sh6 milioni na zinasema zinatoa huduma," amesema Waitara.