Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:57 am

UTAFITI: VITU 6 USIVYO VIJUA KUHUSU KISIWA CHA GUAM NA AMBAVYO VITAKUSHANGAZA

MAREKANI: Sio kila mara unasikia kuhusu kisiwa cha Guam ambacho ndio kikubwa zaidi katika bahari ya Pacific na kinamilikiwa na Marekani.

Kimekuwa katika habari kwa sababu Korea Kaskazini imetishia kushambulia kambi yake ya kijeshi ikiwa ni miongoni mwa mgogoro na Marekani.

Inajiri baada ya rais Donald Trump kusema kuwa taifa hilo linafaa kutarajia vita vikali kutoka kwa Marekani.

Huku Guam ikiangaziwa haya hapa mambo sita unayofaa kujua kuhusu kisiwa hicho.

Ni eneo ambalo liko mbali zaidi kwa raia wa Marekani kutembelea bila kutoka Marekani.


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eneo la Tumon Bay ni maarufu miongoni mwa watalii

Licha kumilikiwa na Marekani, kiko maili 8000 kutoka Marekani na inachukua takriban saa 19 kusafiri kwa ndege kutoka mji wa New York.

Wamarekani wanaweza kuelekea katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.

Kila mtu aliyezaliwa kisiwani Guam ni Mmarekani lakini hawezi kumpigia kura rais.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sherehe inafanyika katika baranara mjini Tumon

Tangu mwisho wa vita vya dunia , watu wawili waliokuwa wakiishi katika kisiwa hicho walipewa uraia lakini hawawezi kumpigia kura rais wa Marekani. Wana mwakilishi mmoja wa serikali laki yeye hana uwezo wowote kuhusu utengenezaji wa sera.

Guam ni kambi muhimu ya kijeshi


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya kijeshi ya Marekani inapaa kutoka Guam

Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya wanamaji na wanaanga

Pia inakadiriwa kwamba karibia asilimia 10 ya watu wa Guam wenye idadi ya 160,000 ni ya wanajeshi.

Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Guam ni kisiwa cha kisasa chenye majumba marefu na maeneo manne ya kitalii

Chamorro ni jina la jumla linalopewa watu wanaoshi katika kisiwa cha Guam na watu wanaoshi katika visiwa vya Micronesia katika bahari ya Pacific.

Utamaduni wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban miaka 300 hadi 1898.

Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tumon ndio wilaya ya kutalii kisiwani Guam

Watalii kutoka Taiwan , Korea Kusini na Japan huchukua saa nne kusafiri hadi katika kisiwa hicho kwa likizo ya kupata jua mbali na kununua vitu ambavyo havilipishwi kodi.

Maduka yote makubwa huuza bidhaa za mitindo na mengi hufunguliwa kwa saa 24 kwa siku.

Ricardo Blas Jr. ndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Blas Jr. akishindana katiika michezo ya olimpiki ya 2012.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mchezaji wa judo ambaye alishiriki judo katika michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba bendera ya Guam katika mashindano yote lakini akashindwa kupata medali licha ya kuwa mhcezaji judo mwenye uzani mzito zaidi wa kilo 214.

#BBCswahili