Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:13 am

UTAFITI: NJIA YA KUMFANYA MSICHANA WAKO AKUPENDE DAIMA

Hizi hapa njia za kufanya mwanamke akupende daima

.1. Ipende familia yake(wazazi, kaka au dada zake) kwa ukaribu. Jaribu kuwaandalia zawadi katika sikuku mbalimbali na kuwaonesha kuwajali. Itamfanya aone unamjali yeye pamoja na familia yake.

2 akiwa katika hali ambayo si nzuri yaani hana raha au kuuziwa na mtu mwingine mtazame machoni ukiwa unatabasamu na umsifie yeye ni msichana mzuri kuliko yeyote aliyewahi kuzaliwa katika hii dunia kisha mkumbatie.

3. Anapoanza kulia usithubutu kuzungumza chochote. Mkumbatie na kuzichezea nywele zake kwa kuzipapasa akiwa kifuani mwako. Hujihisi faraja na kujiona yupo mahala salama kuliko yeyote

4 jitahidi kumpikia chakula akipendacho siku akikutembelea nyumbani kwako ama geto na ukipatie sawa sawa hii itamfanya kukuona wewe ni mvulana unayefaa kuwa mume wake.

5 usizungumze naye sana kuhusu mambo ya kufanya mapenzi, hii itamfanya kukuogopa atahisi una nia ya kumchezea kisha umuache. Kwa mwanamke ambaye upo naye serious hakikisha uligusii sana hili katika uwepo wenu tulivu chumbani labda mara chache mkizidiwa hii itamfanya aone wewe ni mwanaume usiye na tamaa ya ngono.

6 jitahidi kujua vitu ambavyo anapendelea. Mfanyie mara kwa mara vitu hivyo itamfanya kutamani kuwa na wewe muda wote na kukukumbuka pale anapokuwa mbali na wewe.

7 jitahidi kumuuliza mara kwa mara kuhusu siku yake imeendaje kama atakuwa ameboreka na mtu aliyemuuzi mbembeleze kwa kumfariji asiwe na hasira itamfanya kukuambia kila linalomuuzi akiamini furaha pekee ipo kwako.

8 mwanamke hapendi ugomvi kelele na kupigwapigwa hata kama amekuuzi usimkaripie ni heri kama kuna kitu umesikia kaa dakika chache mpaka hasira zipungue kisha ndio umuulize kwa upole atakuona ni mwanaume mwenye busara hivyo hata kama itakuwa ni kweli basi atakueleza ukweli bila kukuficha hii utokana na moyo utamsuta kwa kile alichokifanya ukiwa mpole kwake.

9 kuwa muongeaji sana mwenye hadithi mbalimbali za kuvutia unapokuwa naye. Itamfanya asiatamani kukaa mbali nawe. Sio unakaa kisha unataka yeye ndiye azungumze ataaga mapema na kuona bored utakapokuwa unamuita mara nyingine ataona unamchosha huna story huna jipya.

10. Kuwa mwenye mipango endelevu. Hakikisha ubweteki na kuridhika na hapo ulipo hakikisha unamueleza msichana wako kila unachozani kizuri katika kuwakwamua katika hatua fulani kwenda nyingine itamfanya aone wewe utakuwa baba bora baadaye