Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:28 pm

UTAFITI: MAMBO 8 MAKUBWA YAKUFANYA NAKUTOKUFANYA UKIWA KATIKA MAHUSIANO

Haya ni mambo 8 ya kufanya na kutokufanya ili kuondoa matatizo katika uhusiano wako na kuyapa nguvu mahusiano yako na Mwenza wako.

Kwa hali halisi na mazoea tunaweza kusema kwenye mapenzi kuna kitu kilichomo zaidi ya sanaa ya upendo kuliko tunavyoweza fikiria. Watu ni watata, waliojawa madhaifu na wingi wa tamaa, na wenye kutafuta kueleweka zaidi.

Ukiacha hayo, Mwanadamu pia amejawa na uwezo mkubwa sana kuonyesha upendo endapo wataonyweshwa au kupewa upendo sahihi.

Dhumuni kubwa la mahusiano linatakiwa kuwasaidia tulionao kwenye mahusiano waachie upendo wao mwingi ili tuweze pata mahusiano tunayoyahitaji. (Fulfilling relationship)

Tunaona kila siku kwamba watu wanaendelea kufanya makosa yale yale kila siku kwenye mahusiano na kutegemea kupata majibu tofauti. Mbaya zaidi kukosekana kwa usalama au kutokujiami (insecurities) na tabia mbaya zinapelekea kukufanya mtu atende vitu vinavyopelekea kuharibu kile tunachoweza sema mahusiano yenye afya njema. Watu tofauti tunaokua nao kwenye mahusiano huleta hisia tofauti kwetu, nyingine unaweza hisi hukuwahi kabisa kua nazo kabisa na kudumisha mahusiano kukawa kugumu kwa pande zote mbili. Kwa hili tunatakiwa kuhakikisha tunafanya sehemu yetu.

Sasa tunafanyaje kutatua yote hayo na kuboresha ubora wa upendo wetu: Haya mambo 8 yatakusaidia na kama ukiyafanya yakawa tabia yako, utaimarisha mapenzi yako kwa amani, fahari na furaha.

Kuza hisia za kuwa zaidi ya Rafiki

Watu wengi huishi pamoja kimwili lakini hawako pamoja kihisia. Hisia za zaidi ya kirafiki ni kujua nini mpenzi wako anataka kabla hata ya yeye kupata nafasi ya kukuambia au pia kuchukua hisia zao kama vile ni zako. Unaweza kukuza hizi hisia za zaidi ya urafiki kwa kuwa mkweli kwa mpenzi wako na kuwa mwepesi kusaidia katika analolihitaji.

Panga maisha pamoja.

Plani zetu za maisha zinaweza zisiwe jinsi tunavyozitaka, lakini kwa kuwaza kwa kuangalia maisha yako yatakua vipi badae na mpenzi wako, inahamasisha kuchukua hatua sahihi kudhihirisha mipango yetu ya muda mrefu. Ongelea kuhusu miaka ijayo na pia panga mikakati ya kufikia vitu hivyo mnavyotaka kwa pamoja: yaweza kuwa nyumba, familia, uwekezaji n.k

3. Leta pumziko au faraja.

Mpenzi wako anataka kurudi nyumbani kuliko na upendo na sio maumivu ya kichwa. Tengeneza nyumba yako iwe sehemu inayomfanya mpenzi wako ajisikie amani, imara na sehemu ya kulelewa. Usianze kuongelea kuhusu matatizo yako mara baada ya kuingia mlangoni. Bili, kazi, mkwaruzano mliokua nao asubuhi- hivi vitu vinaweza kusubiri mpaka mazingira sahihi ya ninyi kuyaongelea hayo.

Tenda kwa wakati.

Wakati unaweza kuwa adui yako mkubwa au rafiki yako mkubwa. Katika kila muda, wakati unaweza kuwa upande wako au badala yako. Hekima ni kutambua tu wakati gani utende hiki na wakati gani usubiri kutenda kile.

Ukisikiliza kilicho moyoni mwako unaweza kutambua mawimbi tofauti ya wakati. Usimlazimishe mwezi wako kufanya kitu ndani ya muda fulani, mfano kumsukuma kuoa ndani ya mwaka mmoja, hii ni dhana yako wewe ya wakati sio ya kwake. Chukua hatua kubwa ya kuendelea mbele endapo tu nyote mmekubaliana kufanya hivyo hata kama itachukua muda mwingi kuliko ulivyotaka.

Usitumie udhaifu wao.

Kila siku unauamuzi wa kuchezea udhaifu wa mwenzio au kuimarisha uwezo wao. Kama kila mara wewe huongelea tu kile anachokifanya vibaya mwenzio, hawataweza kupata motisha ya kufanya chochote vizuri. Hamna mahusiano yatakayoweza kushamiri katika mazingira hasi ya namna hiyo.

Kuna njia za kiungwa nyingi tu za kumuelewesha mpenzi wako kipi anapaswa afanye tofauti, na kuwakaripia mara kwa mara sio miongoni mwa hizo njia.

6. Usilipizie / usilipize kisasi

Kwa chochote kile alichofanya mpenzi wako au alikukosea zamani, usilipize kisasi. Dunia ni duara, Weka nafsi yako iwe safi kwa kumtendea mtu kile ambacho wewe akikutendea utafurahi bila kuwaza alikuafanyia nini. Hii ni wajibu wako kwa ajili ya nafsi yako na si kwa mwingine yeyote. Kumbuka, unavyotendewa na mtu ni ‘karma’ yake, unavyomjibu wewe ni ‘karma’ yako.

7. Usidhani au kuzusha vitu nje ya uwiano. (out of proportion)

Kabla hujatupa mpira, kaa chini na tafakari fikra hizo kwa umakini: hivi hiki ni kabaya kiasi hiki? Ongea na mpenzi wako kwa wazi kuhusu kinachokutatiza badala ya kumvamia.

Mara nyingi tunakuza ukali wa jambo kwasababu ya woga na kutokujiamini, wakati kiukweli wala haiko hivyo tunavyofikiria kabisa.

Kabla ya kudhani vitu ambavyo tunahisi vinaweza kuwa vya uongo, jiulize kama ni kweli vina uzito wa kuhatarisha mahusiano yenu.

Usifanye maamuzi kwa pupa. (out of desperation)

Fikiria kwa makini maamuzi yako hata mara elfu moja kabla hujaamua. Maamuzi ya pupa yatazidisha tu matatizo. Kama unataka mpenzi wako abadilike kwa hali yoyote ile, usimtishie kuachana nae wakati kiukweli ni kitu cha mwisho kabisa ambacho ungetaka kufanya. Akikubali kuachana na wewe utajisikia vibaya zaidi. Acha hisia zako zipoe kwanza kabla ya kumfikishia chochote kile, jaribu kila mara kuangalia sababu zilizojificha za kwanini wanafanya wanayofanya kwa wakati huo.

Mahusiano ya mapenzi ni wazi kwamba ni magumu sana kuyatunza kama hatutafata njia sahihi kukubaliana na maadiliko chanya. Chukua haya mambo nane kuondoa matatizo na kuimarisha mapenzi yako na mwezi wako.