- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
UTAFITI: JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA
JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA
Je, wajua kwamba magonjwa mengi ya kuambukizwa huambukizwa kwa njia rahisi sana ambazo unaweza kuzizuia na kuyazuia magonjwa hayo yasikupate? Ni rahisi sana.
Ni muda mrefu sasa watu wengi tumekuwa wahanga wa magonjwa kama vile Malaria, Mafua, Homa ya matumbo, maambukizi katika njia ya mkojo na kadhalika. Hakuna anayependa kuumwa magonjwa haya, isipokuwa tu labda hatujui jinsi ya kujikinga au hatuzingatii mafunzo.
Unakumbuka mara ya mwisho uliumwa ugonjwa gani? Uliupataje?Ulipewa ushauri gani ili kujikinga usiupate tena?
Kuna makundi makuu mawili ya magonjwa
i.Magonjwa ya kuambukizwa
ii.Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa
Hayo magonjwa yote yana namna zake za kujikinga na kuyadhibiti. Upo tayari kujua kuhusu magonjwa ya kuambukizwa ili uweze kujikinga na kuwakinga wengine? Endelea kusoma……
Magonjwa ya kuambukizwa ni magonjwa yanayoweza kumpata mtu kutoka kwa mtu mwingine au mnyama endapo atapata vijidudu vya ugonjwa kutoka kwa mtu au mnyama huyo
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ni magonjwa ambayo hayawezi kumpata mtu kutoka kwa mtu mwingine
Mifano :
Magonjwa ya kuambukizwa – Matende, Malaria, Kipindupindu, Mafua, U.T.I. , Kaswende, Homa ya matumbo (Typhoid) nk
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa – Kisukari, Shinikizo kubwa la damu (High Pressure), Saratani, Magonjwa ya akili nk
JINSI MAGONJWA YANAVYOAMBUKIZWA
1.Kugusana (moja kwa moja au sio moja kwa moja – kuchangia vitana, miswaki, nyembe, sindano, taulo nk) na mgonjwa – Mifano ya magonjwa ni tetekuwanga, mba, ukurutu nk
2.Kugusana kwa kujamiiana – Mifano ya magonjwa ni homa ya ini, kaswende, kisonono, ukimwi nk
3.Kung’atwa na wadudu wanaobeba vijidudu vya magonjwa – Mifano ya magonjwa ni Malaria, Homa ya manjano, Ebola, Malale nk
4.Uchafu kutoka kwenye kinyesi kuingia tena mwilini kupitia mdomoni – Mifano ni homa ya matumbo, kipindupindu nk
5.Vijidudu kujipenyeza kupitia kwenye ngozi yako
6.Kula nyama na bidhaa za wanyama zenye vijidudu vya magonjwa – Mifano ni minyoo, kimeta, kifua kikuu nk
7.Kuvuta hewa na matone yenye vijidudu vya magonjwa – Mifano ya magonjwa ni kifua kikuu, mafua, mafua ya ndege nk
8.Kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto – Mifano ni kaswende, ukimwi, kisonono nk
JINSI YA KUZUIA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA
Tunaweza kuzuia magonjwa ya kuambukizwa yasiambukizwe zaidi na kuenea kwa
i.Kukikabili chanzo cha ugonjwa au mgonjwa
ii. Kuvuruga njia ya kusambazwa kwa ugonjwa na kuzuia isifanikiwe kusambaza ugonjwa
iii. Kujikinga na kumlinda mtu ambaye haumwi lakini anaweza kupata ugonjwa
iv. Elimu na Ushauri wa Afya kwa jamii
KUKIKABILI CHANZO CHA UGONJWA AU MGONJWA
i.Matibabu sahihi na ya haraka – Mfano Kifua kikuu, Magonjwa ya macho,
ii.Kumtenga ili asiambukize wengine – Mfano Ebola, Kipindupindu, Tetekuwanga nk
iii.Kukabili wanyama na mazingira yanayohifadhi vijidudu vya magonjwa – Mifano ni nyani, madimbwi ya maji, vichaka nk
iv.Kutoa taarifa na elimu kwa umma juu ya kujikinga dhidi ya chanzo cha ugonjwa
KUVURUGA NJIA ZA KUSAMBAZWA KWA UGONJWA
i.Kufanya usafi wa kutosha wa makazi na mazingira yetu
ii.Kufanya usafi wa kutosha wa mwili na kubadili tabia zetu ambazo zinaweza kutusababishia kuambukizwa magonjwa
iii.Kuua wadudu wanaoeneza vijidudu vya magonjwa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine
iv.Kuua kabisa vijidudu kwa kutumia kemikali na njia nyingine za kuulia vijidudu katika vyombo, nguo, sindano, nyembe, vitana nk
MAMBO YA KUFANYA ILI KUJIKINGA DHIDI YA MAGONJWA NA KUWA NA AFYA NJEMA
i.Epuka misongamano mikubwa ya watu
ii.Hakikisha usafi binafsi wa mwili, mavazi, vyombo na mazingira
iii.Haribu mazingira yote ya wadudu na vijidudu vinavyoeneza magonjwa kuzaliana na kuwepo katika mazingira yako
iv.Epuka kugusana na mgonjwa anayeweza kukuambukiza kwa njia ya kugusana pamoja na kuchangia vitu vinavyoweza kueneza magonjwa
v. Hakikisha unafunga pua na mdomo wako enapo kutakuwa na mtu anakohoa au kupiga chafya bila kufunika pua na mdomo wake
vi. Kufanya mazoezi ya kutosha na kula chakula bora
vii. Jiepushe na ngono isiyo salama
viii. Hakikisha usafi na usalama wa maji ya kunywa na vyakula pamoja na mazingira na vyombo unapokula chakula na kunywa maji
ix. Jikinge using’atwe na wadudu wanaosababisha magonjwa na wanaoeneza vijidudu vya magonjwa