- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
UTAFITI: HIZI HAPA SABABU ZA WANAWAKE KUSHINDWA KUTUNZA SIRI
Kwa kawaida wanawake wanamajukumu mengi sana kuliko wanaume. Kuna suala la kulea watoto, kulea wazee au ndugu wa familia, kuna suala la kujua familia itakula nini, nini hakipo na vituvya namna hiyo.
Kuna yale majukumu ya nje na ya nyumbani kama shambani, kazini au kwenye shughuli za uzalishaji. Kwa ujumla,iwe mwanamke ana shughuli za nyumbani peke yake au za nyumbani na nje yanyumbani, bado ni wazi ana majukumu mengi zaidi.
Tafiti nyingi zinaonyesha tofauti mbili kubwa zilizopo kati ya wanaume na wanawake, hasa kuhusiana na kusongekakiakili. Tofauti hizi zinaonyesha ni kwa nini mwanamke husongeka zaidi kiakilikuliko mwanaume.
Kwanza ni kwamba, wanawake hupambana na mambo, matukio au vitu vingi vyenye kusongesha na kusononesha,kuliko wanaume.
Mambo matukio au vitu hivyo ni pamoja na shida za ndoa. Kukandamizwa katika maeneo ya kazi, ugumu wa kipato na mengine mengi.
Pili ni kwamba, wanawake hujali au huzipokea kirahisi athari za msongo au sononi za maisha kuliko ilivyo kwa mwanaume .Hata hivyo miili ya wanaume naile ya wanawake huathirika kwa kiwango sawa, kutokana na sononi au misongo yakimaisha. Mwili wowote wa mwanamke au mwanaume, unapopokea msongo kutoka katika hisia, hufanya mabadiliko ilikukabili msongo au sononi hiyo.
Lakini ni kwa namna gani kihisia tunajibu misongo au sononi za kimaisha, kuna tofauti kati ya wanaume na wanawake. Wanawake kwa upande wao wanapokuwa kwenye sononi au kusongeka hupenda kuwa karibu na wengine au kujenga urafiki. Ikiwa ni kama njia ya kujikinga nahali hiyo.Ndiyo maana wanawake wanapokuwa kwenye matatizo mengi yenye kuwasonga hususan ya ndoa au mahusiano, hupenda kuyasema sana kwa wenzao, ambapo wanaume hudhani wanawake hawana siri. Kuyasema hayo matatizo kwa wenzao, huwapa wanawake nafuu ya aina fulani.
Kwa kuwa pamoja na wengine au rafiki zake, mwanamke mwenye sononi au aliyesongeka huhisi nafuu sana na hupata ahuweni kwa kuona kwamba, ana watu wanaoweza kumsikiliza. hii humsaidia kuwezakumudu kupita vizuri katika kipindi hicho cha msongo au sononi, hasa kama nicha muda.
Lakini pia kwa kuwa na wenzake nakueleza yale yanayomsibu na wenzake wanapompa moyo anajenga kujiamini zaidi. Kujiamini ni kipengele muhimu sanakatika kumfanya mtu kuondoka kwenye kusongeka au kusononeka.
Kwa kawaida tunaposhindwa kujiamini huwa tunaona kwamba, maisha ni kitu kisicho na maana sana. Hivyo tukianza kujenga kujiamini, tunaanza kuhisi kwamba, maisha yana maana na matatizo yetu ni sehemu ya maisha hayo.Siyo lazima mwanamke awe na marafiki wengi au ajenge urafiki ili kupata watu wa kumsaidia kuondoka kwenyesononi, hapana. Jirani anayeaminika, mume, ndugu, wazazi au watumishi wenzakena hata vikundi vya dini yake vinaweza kumsaidia kuondoka kwenye sononI.