Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:48 pm

UTAFITI: HAYA HAPA MATATIZO YA KUPENDA KUPITA KIASI

Kupenda ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu, kwa sababu asilimia kubwa ya matendo ya mtu huongozwa na mapenzi.



Baadhi yetu tuko tayari kupoteza maisha kama tutaachwa na wapenzi au kukosa mambo tuliyoyapenda.

Kupenda kwa kiwango cha kushindwa kujizuia na kuvumilia ni hatari kwa afya ya mwanadamu.

Kisaikolojia ni kuutesa moyo kwa sababu mpenzi wako kakukataa ni matokeo ya kufikiri vibaya kwani ushahidi uliopo miongoni mwetu unaonesha kuwa mapenzi si kitu cha kudumu kwa miaka mingi na anayesema anaweza kupenda jambo moja milele kwa kiwango kilekile ni mtu anayejiwekea mtego utakaomnasa mwenyewe na kumtesa.