Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:38 am

Uchaguzi Ufaransa Emmanuel Macron na Marine Le Pen waongoza duru ya kwanza

Ufaransa:Mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa nchi hiyo, huku dalili zikionyesha, baada ya wiki mbili atapambana katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front. Aboubakar Famau na taarifa zaidi:

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka thelathini.

"Nimesikia katika miezi iliyopita na leo tena, shaka, hasira na uoga waliokuwa nao wafaransa. Na hamu ya mabadiliko. Hiki ndicho kilichowasukuma kuacha vyama vikuu viwili vilivyotawala kwa zaidi ya miaka thelathini.")

Ameongeza kusema kazi yake hivi sasa ni kuipatanisha nchi na kuunganisha nguvu kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi."wiki mbili kuanzia sasa, nataka niwe rais wenu. (CROWD CHEERING) Rais wa raia wote wa ufaransa. Rais wa wapenda nchi dhidi ya vitisho vya wanaotaka kujitenga.")

Kwa upande wake, Le Pen ameyaelezea matokeo hayo kuwa ni ya kihistoria. Huku akijiita kuwa yeye ni ndio chaguo la wafaransa na kusema kuwa muda umefika wa kuwabadilisha watu.

"Wakati umefika wa kuwaweka huru raia wa ufaransa na jamii yote wa rais wa Ufaransa bila kusahau marafiki zetu walio nje ambao wameniamini na naona fahari kwa imani walioonyesha kwangu.")

Rais wa ufaransa amempigia simu bwana Macron na kumpongeza, bila kuonyesha kumuunga mkono rasmi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafuasi wa Bw Macron wakisherehekea...

Mmoja wa wasaidizi amesema haikuna vigumu kujua chaguo lake kati ya waziri aliyefanya kazi nae na mwakilishi mwenye mrengo wa kulia.

Francois Fillon ambae ni mgombea wa mrengo wa kati, na aliyewahi kuwa waziri mkuu, ambae pia aliwahi kukabiliwa na tuhuma za ufisadi, wakati akiwahutubia wafuasi wake amesema atampigia kura Macron.

Wakati hayo yakijiri, kumetokea vurugu katikati mwa jiji la Paris zilizohusisha vijana wenye mrengo wa kushoto ambao hawakufurahishwa na ushindi wa Le Pen.

Polisi walipambana nao kwa kuwapiga viboko.Vile vile kumekuwa na maandamano magharibi mwa mji wa Nantes.

Tayari viongozi mbali mbali wa nchi za ulaya wameanza kuonyesha kumuunga mkono Macron.

Msemaji wa Chancellor wa ujerumani Angela Merkel amemtakia kila la heri, na kusifu msimamo wake kuunga mkono Umoja wa Ulaya.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafuasi wa Marine Le Pen nao wakisherehekea

Hata hivyo, Le Pen pia amepata kuungwa mkono kutoka jamii ya kimataifa ambapo mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa mambo ya nje.