- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TRUMP: CORONA IMEISHAMBULIA MAREKANI KULIKO SHAMBULIO LA SEPTEMBA 11
Rais Donald Trump wa Marekani amewaambia waandishi habari mjini Washington kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeiathrii Marekani kwa kiwango kikubwa kuliko mashambulizi ya tukio la kigaidi la Septemba 11 yaliyofanywa na Osama Bin Ladeni au mabomu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pearl Harbor ya mwaka 1941.
Hayo ni moja ya matukio makubwa kabisa na yaliyosababisha athari pana katika historia ya Marekani ndangu kuumbwa kwake.
Mashambulizi ya Japan kwenye kambi ya Pearl Harbor iliyokuwepo Hawaii yaliilazimisha Marekani kuingia katika vita kuu ya pili ya dunia huku mkasa wa Septemba 11 uliwauwa wamarekani zaidi ya 3,000 na kuisukuma Washington kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi nchini Iraq, Afghanistan na kwingineno.
"Tumepatwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwetu.
"Shambulio hili ni baya zaidi ya la Bandari ya Pearl. Hili baya zaidi ya la Kituo cha Biashara cha Dunia (9/11). Hatujawahi kupatwa na shambuli kama hili.
"Na halikutakiwa kutokea. Lingeweza kuzuilika kwenye chanzo chake. Lingeweza kuzuiliwa na Uchina. Lingeweza kuzuiliwa kwenye chanzo chake, lakini hilo halikufanyika." amesema Trump
Trump ameilaumu China akisema virusi vya corona visingesababisha athari kubwa iwapo Beijing ingefanikiwa kuvidhibiti kikamilifu vilipozuka mwishoni mwa mwaka uliopita.
Huo ni mfululizo wa lawama za Marekani kwa China kuhusu virusi vya corona na katika siku za karibuni rais Trump na viongozi wake waandamizi wamesema wana ushahidi kuwa virusi vya corona vilizuka kutoka maabara moja mjini Wuhan nchini China.
Madai hayo yamepingwa vikali na China na wanasayansi bado wanaamini virusi hivyo vialinzia kwa wanyama kabla ya kuingia kwa binadamu hususan kupitia soko la nyamapori la mjini Wuhan.
Uchina hata hivyo inasema kuwa Marekani inataka kuitumia kama njia ya kuficha mapungufu yao ya nmana gani wamelishughulikua janga hilo.
Toka janga hilo lilipuke katika Mji wa Wuhan mwezi Disemba, virusi vya corona tayari vimeshathibitishwa kuwapata zaidi ya watu milioni 1.2 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 73,000 nchini Marekani pekee.
Hadi sasa zaidi ya watu 73,000 wamekufa nchini Marekani kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na mkuu wa zamani wa taasisi ya kuzuia magonjwa nchini humo amebashiri idadi ya vifo inaweza kufikia 100,000 mwishoni mwa mwezi Mei.
Tom Frieden ametaka wabunge kujitayarisha kwa vita ngumu na ya muda mrefu ya kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19 ma ametoa wito wa kuongeza uwezo wa kufanya vipimo.
Hadi sasa virusi vya corona vimesababisha vifo vya watu 260,000 kote duniani huku wengine karibu milioni 3.7 wameambukizwa maradhi ya COVID-19.